Mohammed Ra'ad, mkuu wa mrengo wa Hizbullah katika bunge la Lebanon, amesema kuwa, chama hicho kiko tayari kukubali muundo wowote unaoweza kulinda nchi dhidi ya vitisho na hatari zilizopo za adui.
Usitishaji vita huo unatekelezwa katika hali ambayo utawala wa Kizayuni haujaweza kuvishinda vikosi vya Hizbullah na kuzuia mashambulizi ya roketi na makombora ndani kabisa ya ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) licha ya miezi kadhaa ya mashambulizi makubwa ya anga na ardhini.
Usitishaji vita huo unatekelezwa katika hali ambayo utawala wa Kizayuni haujaweza kuvishinda vikosi vya Muqawama wa Kiislamu wa Lebanon na kuzuia mashambulizi ya roketi na makombora ndani kabisa ya ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) licha ya miezi kadhaa ya mashambulizi makubwa ya anga na ardhini.
Ni kutokana na sababu hiyo ndio maana, tangazo la usitishaji vita huo limepokewa kwa hisia hasi na aghalabu ya wanasiasa wa Kizayuni, na wapinzani wa Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni ambao wamekiri kwamba, kukubali usitishaji vita huo kunaonyesha kushindwa kikamilifu jeshi la utawala huo dhidi ya Hizbullah ya Lebanon.
Wazayuni wakasirika
Yair Lapid, kiongozi wa upinzani anayepinga baraza la mawaziri la Netanyahu, ameandika ujumbe katika mtandao wa kijamii wa X: "Baraza la mawaziri la Netanyahu limelazimika kukubali usitishaji vita na Hizbollah, na Netanyahu ameshindwa kugeuza mafanikio ya kijeshi kuwa ushindi wa kisiasa."
Naftali Bennett, Waziri Mkuu wa zamani wa utawala wa Kizayuni pia ameyatathmini makubaliano hayo ya usitishaji vita kuwa ni piigo na kushindwa kabisa Netanyahu katika uga wa diplomasia na usalama.
Matokeo ya uchunguzi wa maoni uliofanywa na Kanali ya 13 ya Televisheni ya utawala wa Kizayuni pia yanaonesha kuwa, asilimia 61 ya wakaazi wa ardhi zinazokaliwa kwa mabavu wanaamini kuwa, jeshi la utawala huo ghasibu halijapata ushindi.
Vita vilianzaje?
Tangu tarehe 7 Oktoba 2023, kwa uungaji mkono kamili wa nchi za Magharibi, utawala wa Kizayuni umefanya mauaji makubwa katika Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan dhidi ya wananchi wasio na ulinzi na madhulumu wa Palestina.
Baada ya hapo, Israel ilishambulia kusini mwa Lebanon na kuua idadi kubwa ya raia. Kimya cha jamii ya kimataifa na taasisi za kutetea haki za binadamu kuhusiana na jinai za utawala huo ghasibu kimesababisha kuendelea vitendo vya kinyama na vya kikatili vya utawala wa Kizayuni vya kuwaua wanawake na watoto wa Kipalestina na Lebanon.
Hizbullah ya Lebanon nayo haikunyamaza kimya mbele ya kulengwa kwa raia wa nchi hiyo na Ukanda wa Gaza, na ilitekeleza operesheni nyingi dhidi ya maeneo na vitongoji vya walowezi wa Kizayuni kaskazini mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu, ambayo iliendelea hadi Jumatano asubuhi ya leo na kabla ya usitishaji vita kuanza kutekelezwa. Suala hili linaonyesha wazi kwamba, pamoja na madai ya mamlaka ya Kizayuni, Hizbullah bado ina nguvu ya kuendeleza mapambano dhidi ya utawala wa Kizayuni.
Israel imelazimika
Katika upande mwingine, Israel imelazimika kukubali usitishaji vita katika hali ambayo siasa za ndani za utawala wa Kizayuni zilikuwa zikizidi kukosolewa, na wakati huo huo malengo ya baraza la mawaziri la Netanyahu huko Gaza hayajafikiwa. Kwa muktadha huo, Netanyahu anaona usitishaji vita nchini Lebanon kuwa ni fursa ya kisiasa na kiusalama kwa minajili ya kupunguza migogoro ya ndani na nje ya Israel.
Pamoja na hayo, vikosi vya muqawama vimeonyesha madhihirisho tofauti ya uwezo wao dhidi ya adui Mzayuni na kuthibitisha kuwa, endapo utawala wa Kizayuni utafanya kosa na kuzusha mgogoro, vina uwezo wa kukabiliana na chokochoko za Wazayuni.
Esmail Beqaei, msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran pia ameashiria misimamo ya mara kwa mara ya Tehran kuhusiana na ulazima wa kusimamisha mara moja vita dhidi ya Gaza na Lebanon na hatua kubwa za kidiplomasia za Iran za kufikia lengo hilo katika kipindi cha miezi 14 iliyopita na kueleza kwamba:
Natija ya uchochezi wa vita na jinai za utawala wa Kizayuni ambao umeambatana na uungaji mkono kamili wa Marekani na baadhi ya serikali za Ulaya ni kuuawa shahidi watu 60,000 wasio na hatia, kujeruhiwa watu 120,000, na kuyahama makaazi yao watu milioni tatu na nusu waliodhulumiwa wa Palestina na Lebanon, na kusababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu muhimu katika Ukanda wa Gaza na Lebanon.
3490845