Hizbullah iliweka picha ya shakhsia huyo anayeheshimika kwenye kaburi lake kwenye Makaburi ya Rawdhat al-Hura katika viunga vya kusini mwa Beirut.
Shahidi Safieddine aliuawa, pamoja na idadi ya masahaba zake, katika shambulio la Israeli kwenye vitongoji vya kusini mwa Beirut mnamo Oktoba 3, 2024.
Alitarajiwa sana kuchaguliwa rasmi kama katibu mkuu wa Hizbullah baada ya kuuawa shahidi Sayed Hassan Nasrallah.
Shahidi Safieddine alijiunga na Hizbullah mwaka 1982 na aliwahi kuwa mkuu wa Halmashauri Kuu yake kuanzia 1994 hadi kifo chake cha kishahidi.
Tangu 2017, alikuwa amewekwa katika orodha ya wanaosakwa na Marekani kutokana na nafasi yake muhimu katika mapambano dhidi ya utawala wa Kizayuni.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Hizbullah baada ya kuuawa shahidi, Safieddine alitumia maisha yake yote ya heshima kutafuta uhuru wa Quds tukufu na kulinda heshima na mipaka ya Lebanon dhidi ya uvamizi na jinai za utawala ghasibu wa Kizayuni, na hatimaye aliuawa shahidi kwenye njia hii takatifu.
4252841