Katika taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti yake rasmi siku ya Jumatano, wizara hiyo ilimpongeza Safieddine kwa kutumia maisha yake yote kwa ajili ya kuukomboa mji mtakatifu wa al-Quds (Jerusalem) uliko Msikiti wa Al Aqsa.
Aidha taarifa hiyo imelaani hujuma ya kigaidi ya utawala ghasibu wa Israel iliypelekea kuuawa shahidi kiongozi huyo mkuu wa Hizbullah.
Wizara hiyo imetoa pole kwa familia ya mashahidi, watu wa kieneo na makundi ya muqawama, mataifa ya Kiislamu duniani, na Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyed Ali Khamenei.
Taarifa hiyo imelaani ukatili huo wa Israel na kuutaja kuwa "uhalifu usiosameheka," huku pia ikilaumu "ushirikiano wa moja kwa moja wa serikali ya Marekani na serikali nyingine zinazounga mkono utawala ghasibu wa Israel katika uhalifu huu."
Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imesisitiza kwamba “bila shaka, kuuawa shahidi kwa viongozi wa muqawama hakutadhoofisha hata chembe moja ya azimio, imani, na utashi wa makamanda na wapiganaji wenye bidii wa muqawama, na mataifa huru ya Kiislamu ya eneo la mapambano dhidi ya uvamizi, ukandamizaji na uchokozi wa utawala wa Kizayuni."
Mapambano hayo, imeongeza wizara hiyo, yataendelea hadi Wazayuni maghasibu watakapotimiliwa na ardhi wa Palestina kukoombolewa.
Taarifa hiy imemsifu shahidi Safieddine kama mmoja wa viongozi na waanzilishi wa Hizbullah, na sahaba wa karibu na mwaminifu wa Katibu Mkuu wa harakati hiyo Sayed Hassan Nasrallah, ambaye aliuawa shahidi wakati wa mashambulizi ya kigaidi ya Israel dhidi ya mji mkuu wa Lebanon Beirut mwishoni mwa Septemba.
Shahidi afieddine "alitumia maisha yake yote ya heshima kutafuta uhuru wa al-Quds tukufu na kulinda heshima na utimilifu wa ardhi ya Lebanon dhidi ya uvamizi na jinai za utawala unaokaliwa kwa mabavu wa Kizayuni, na hatimaye aliuawa shahidi katika njia hiyo takatifu," taarifa hiyo ilibainisha.
Hizbullah ilithibitisha kuuawa shahidi kwa kiongozi huyo mwandamizi katika taarifa yake ya siku ya Jumatano, ikisema kwamba alifikia daraja ya kuuawa shahidi katika "shambulio la kikatili na la kichokozi la anga la Wazayuni."
Safieddine alitarajiwa kuchaguliwa rasmi kama katibu mkuu ajaye wa Hizbullah baada ya Nasrallah kuuawa shahidi.
Utawala wa Israel umezidisha mashambulizi yake ya mauaji ya kimbari dhidi ya Lebanon tangu Oktoba mwaka jana baada ya kuanzisha vita vya mauaji ya halaiki katika Ukanda wa Gaza.
Takriban watu 2,574 wa Lebanon wameuawa kutokana na uvamizi huo.
Hizbullah imekuwa ikijibu ukatili huo kwa kuvurumisha mamia ya makombora mashambulizi dhidi ya ngome za kijeshi na kijasusi za Israel katka hatua ya kuilinda Lebanon na kuwaunga mkono wananchi wa Gaza waliokumbwa na vita.
Hizbullah imeapa kuendelea kulipiza kisasi hadi utawala utakapokomesha uchokozi na mauaji ya kimbari.
Wakati wa kuthibitisha kifo cha kishahidi cha Safieddine, Hizbullah ilimuahidi yeye na mashahidi wenzake kwamba itaendeleza njia ya muqawamana jihadi hadi malengo ya uhuru na ushindi yatimizwe."
3490407