
Kwa mujibu wa kitengo cha kisiasa cha Shirika la Habari la Fars, Ayatullah Khamenei, ametoa ujumbe muhimu kuhusu matukio yaliyojiri hivi karibuni nchini Lebanon.
Ujumbe kamili wa Kiongozi wa Mapinduzi ni huu ufuatao:
Kwa Jina la Allah, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu
Mauaji ya watu wasio na ulinzi nchini Lebanon, kwa upande mmoja, yamewadhihirishia kwa mara nyingine tena watu wote khulka ya kinyama na kihayawani ya Wazayuni; na kwa upande mwingine yamethibitisha uono finyu na sera za kijinga za viongozi wa utawala huo ghasibu.
Genge la kigaidi na mauaji linalotawala utawala wa Kizayuni halijajifunza kutokana na vita vyake vya kijinai vilivyodumu kwa mwaka mmoja huko Ghaza na halijaweza kuelewa kwamba mauaji ya umati ya wanawake, watoto na raia wa kawaida hayawezi kuathiri muundo imara na madhubuti wa taasisi ya Muqawama na kuusambaratisha.
Sasa hivi wanaijaribu tena sera ile ile ya kipumbavu nchini Lebanon. Wahalifu hao wa Kizayuni inawapasa wajue kwamba wao si lolote si chochote kuweza kuasababishia madhara makubwa muundo imara wa Hizbullah ya Lebanon. Vikosi vyote vya Muqawama vya eneo viko bega kwa bega na Hizbullah na vinaiunga mkono.
Hatima ya eneo hili itaamuliwa na vikosi vya Muqawama vikiongozwa Hizbullah ya kujivunia.
Wananchi wa Lebanon hawajasahau kwamba kuna siku, wanajeshi wa utawala ghasibu walifika hadi ya kuiponda ponda hata Beirut, na ni Hizbullah ndiyo iliyokata maguu yao na kuifanya Lebanon iwe ya kuheshimika na kujivunia.
Hata leo hii pia, kwa taufiki na uwezo wa Mwenyezi Mungu, Lebanon itamjutisha na kumdhalilisha adui khabithi na mvamizi.
Ni wajibu kwa Waislamu wote, kwa suhula walizonazo, kusimama bega kwa bega na wananchi wa Lebanon na Hizbullah ya kujivuunia, na kuisaidia katika kukabiliana na utawala ghasibu, dhalimu na khabithi.
Amani iwe juu ya waja wema wa Allah
Sayyid Ali Khamenei
Mehr 7,1403
4239118