IQNA

Muqawama

Shahidi Nasrallah alikuwa Mja wa Kweli wa Mwenyezi Mungu

16:44 - November 10, 2024
Habari ID: 3479731
IQNA – Mwanazuoni mmoja wa Iran ameangazia namna Katibu Mkuu wa zamani wa Hizbullah Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah alivyokuwa amejikurubisha kwa Qur'ani Tukufu, huku akimtaja kama mja wa kweli wa Mwenyezi Mungu.

Akizungumza na IQNA, Hujjatul Islam Seyed Mostafa Hosseini Neyshabouri, Mkuu wa Kituo cha Kimataifa cha Qur'ani na Uenezi cha Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu (ICRO) amesema kuwa, ukuruba wa Nasrallah na Qur'ani Tukufu ulimsaidia kubaki imara katika njia ya Mwenyezi Mungu.

Pia aliashiria sifa ya  Sharh Sadr ya Nasrallah (kufunguka kwa kifua (nafsi), ambayo inaashiria ujasiri na subira ya mtu), akisema hakuna mtu anayeweza kuwa na Sharh Sadr isipokuwa yeye ni Mwislamu wa kweli na amenyenyekea kwa Mungu.

Mwenyezi Mungu anasema katika Aya ya 22 ya Surah Az-Zumar, " Je! Yule ambaye Mwenyezi Mungu amemfungulia kifua chake kwa Uislamu, na akawa yuko kwenye nuru itokayo kwa Mola wake Mlezi (ni sawa na mwenye moyo mgumu?) Basi ole wao wenye nyoyo ngumu zisio mkumbuka Mwenyezi Mungu! Hao wamo katika upotofu wa dhaahiri." Hujjatul Islam Hosseini Neyshabouri ameashiria aya hiyo na kuongeza kuwa Shahidi Nasrallah alipata Sharh Sadr wakati wa mapambano dhidi ya adui.

Amesema busara na hekima ni miongoni mwa sifa nyingine za Shahidi Nasrallah zilizomsaidia katika kupata ushindi na mafanikio.

Akabainisha kwamba kwa mujibu wa Aya ya 269 ya Surah Al-Baqarah, “Humpa hikima amtakaye, na aliyepewa hikima amepewa kheri nyingi.”

Shahidi Nasrallah pia alikuwa na nguvu sana katika suala la usimamizi wa kimkakati, ambao ni muhimu hasa wakati wa migogoro na hii ilisaidia katika ulinzi wa ardhi ya Lebanon na mipaka ya Kiislamu, alisema.

Ushujaa na ujasiri pia vilikuwa vyema katika tabia ya Shahidi Nasrallah na hakuwa na hofu ya mlaumu yeyote, kwa mujibu wa Khatibu aliyenukuu Aya ya 54 ya Surah Al-Maidah, “Enyi mlio amini! Atakaye iacha miongoni mwenu Dini yake, basi Mwenyezi Mungu atakuja leta watu anao wapenda nao wanampenda, wanyenyekevu kwa Waumini na wenye nguvu juu ya makafiri, wanapigania Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu, wala hawaogopi lawama ya anaye laumu. Hiyo ndiyo fadhila ya Mwenyezi Mungu, humpa amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mkunjufu na Mwenye kujua.”

Sayyid Hassan Nasrallah aliuawa shahidi katika shambulizi kubwa la anga ambalo Israel ilianzisha kusini mwa Beirut mnamo Septemba 27 kwa kutumia mabomu ya kivita yaliyotolewa na Marekani.

Mashambulizi ya Israel dhidi ya lebanon yanakuja dhidi ya hali ya mvutano ulioongezeka kati ya vuguvugu la upinzani la Lebanon na kundi linaloikalia kwa mabavu, ambalo lilijumuisha mauaji yaliyolengwa ya makamanda wakuu wa Hizbullah na kulipuliwa kwa vifaa vya mawasiliano vya kundi la muqawama la Waislamu.

3490616

Habari zinazohusiana
captcha