Katika ajali mbaya iliyotokea tarehe 11 Disemba, Bi. Suad Rajab Al-Mazin na mama yake walipoteza maisha walipokuwa wakirejea kutoka katika awamu ya awali ya Mashindano ya 8 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Port Said.
Sasa, kamati ya maandalizi imetangaza jina lake miongoni mwa washindi wa awamu ya awali ya shindano hilo katika kategoria ya kuhifadhi Qur'ani nzima.
Suad alitakiwa kushindana na wavulana na wasichana wengine 22 katika raundi ya mwisho ya kitengo hiki mnamo Desemba 18.
Alikuwa mwanafunzi wa shule kutoka Kijiji cha Adfina katika Jimbo la Beheira kaskazini mwa Misri.
Qiraa na hifdhi yake ya kupendeza katika duru ya awali ilivutia jopo la majaji, na kumfanya kuwa mmoja wa waliopendekezwa kushinda nafasi ya kwanza.
Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar cha Misri, Waziri wa Awqaf wa nchi hiyo na maafisa wengine kadhaa na mashirika ya kidini wametoa risala za rambirambi baada ya kifo cha mhifadhi huyo mdogo wa Qur'ani.
3491097