IQNA

Teknolojia katika Uislamu

Jukwaa la Kujadili Matumizi ya Akili Mnemba au AI Misikitini

20:49 - December 24, 2024
Habari ID: 3479947
IQNA - Kongamano litafanyika katika Msikiti wa Jamkaran huko Qom, Iran, kujadili mahitaji na matumizi ya akili mnemba yaani Artificial Intelligence (AI) katika misikiti.

Makao Makuu ya Kimkakati ya Vyuo Vikuu vya  Kiislamu  (Hauza) ya teknolojia mahiri Smart Technologies yataandaa kongamano hilo maalum siku ya Alhamisi.

Mashirika na taasisi kadhaa kama vile Astan Quds Razavi, Makao Makuu ya Kimkakati ya Misikiti, Kituo cha Teknolojia ya Habari cha Hauza na Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (bunge la Iran) zitashirikiana katika kufanya hafla hiyo.

Wazungumzaji watajumuisha Hujjatul-Islam Ojaghnejad, msimamizi wa Msikiti wa Jamkaran, Reza Taqipour, mkuu wa Kamati ya Akili Mnemba ya Bunge, na Hujjatul-Islam Mohammad Mehdi Moslemifar, katibu wa Makao Makuu ya Mikakati ya Misikiti.

Katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na juhudi za kuchunguza matumizi ya AI katika Hauza na vituo vya kidini.

Vituo vya Kiislamu nchini Iran vimekuwa vikikumbatia akili mnemba ili kusaidia katika uenezaji wa mafundisho ya kidini.

3491186

Kishikizo: akili uislamu
captcha