IQNA

Huduma za kidijitali zinazotumia Akili Mnemba kuwasaidia Mahujaji

23:19 - May 06, 2025
Habari ID: 3480645
IQNA – Mpango mpana wa uendeshaji kwa msimu wa Hija utazinduliwa nchini Saudi Arabia, huku tangazo rasmi likipangwa kutolewa Alhamisi. 

Urais Mkuu wa Masuala ya Msikiti Mkuu wa Makka na Msikiti wa Mtume huko Madina utazindua mpango huo  wa teknolojia ya kisasa.

Mpango huu umeelezewa kuwa wa ukuzaji mkubwa zaidi tangu kuanzishwa kwa mifumo mipya ya udhibiti, huku mkakati wa mwaka huu ukilenga huduma zinazojielekeza kwa Mahujaji, kwa lengo la kuwahudumia mamilioni ya waumini wanaotarajiwa wakati wa Hija.

Mpango huu unalenga kuinua kiwango cha  safari takatifu ya Hija kwa kutumia zana za Akili Mnemba (AI), teknolojia mahiri, na anuwai ya majukwaa ya kidijitali yaliyoundwa kuwaongoza Mahujaji kwa urahisi  na uwazi.

Katika taarifa kwenye akaunti yake rasmi ya X (zamani Twitter), Urais huo umefichua kuwa muundo wa uendeshaji utajumuisha uzinduzi wa mkusanyo wa huduma za kidijitali mahiri wa kina zaidi katika historia ya Hija. 

Mambo muhimu yanayojumuishwa ni: 

- “Manarah 2” Roboti ya AI:  Roboti hii ya kizazi cha pili yenye lugha nyingi  imeundwa kuwahudumia na kuwaongoza Mahujaji. 

- Skrini Mahiri za Lugha Nyingi:  Skrini mahiri (smart screen) zimewekwa katika maeneo muhimu ili kutoa taarifa na msaada wa papo hapo. 

- Jukwaa la Kidijitali la Qur’ani: Jukwaa la hili la kimataifa linasaidia usomaji na kujifunza Qur’ani kwa Mahujaji duniani kote. 

- Programu ya Surat Al-Fatiha:  Programu hii ya kidijitali inapatikana kwa lugha nyingi ili kuboresha uelewa na kushiriki katika moja ya sura zinazosomewa zaidi za Qur’ani. 

- Miradi Maalumu: Programu zinazotoa msaada wa kidini, kiakili, na kielimu kulingana na asili mbalimbali za washiriki wa Hija 

Sheikh Abdulrahman Al Sudais, Mkuu wa Masuala ya Kidini wa Msikiti Mkuu na Msikiti wa Mtume, amesema kuwa mpango wa uendeshaji umejikita katika misingi ya huruma, utulivu, na huduma. 

Ameongeza kuwa lengo ni kuhakikisha Mahujaji wanatekeleza Hija kwa mujibu wa mafundisho ya Mtume Muhammad(SAW) na kwa viwango vya juu zaidi vya uangalizi. 

A Saudi man works on a smart sterilising robot at the Grand Mosque in of Mecca during the Hajj pilgrimage.

3492956

Kishikizo: akili hija teknolojia
captcha