IQNA

Maonyesho ya Pili ya Sanaa ya Qur’an kwa Teknolojia ya AI Yafunguliwa Tehran

14:37 - November 23, 2025
Habari ID: 3481562
IQNA – Maonyesho ya pili ya kazi za Qur’ani Tukufu zilizotengenezwa kwa teknolojia ya Akili Mnemba (AI) yamezinduliwa mjini Tehran, yakionyesha kazi 100 zilizochaguliwa kutoka kwa vijana na chipukizi.

Kituo cha Bagh-e-Honar (Bustani ya Sanaa) ndicho mwenyeji wa tukio hili, likiandaliwa na Klabu ya Sanaa ya AI.

Maonyesho haya yanaonyesha tena uhusiano kati ya sanaa ya kidini, ubunifu wa kizazi kipya, na teknolojia za kisasa.

Baada ya kufanikisha toleo la kwanza na mapokezi makubwa ya kazi za Qur’ani Tukufu zilizotengenezwa kwa Akili Mnemba , safari hii maonyesho ya pili yamefanyika yakionyesha kazi 100 zilizochaguliwa kutoka kwa vijana na chipukizi.

Kazi hizi zinaashiria kukomaa kwa mwelekeo mpya katika uchoraji wa kidijitali wa aya za Qur’ani Tukufu.

Mkusanyiko huu ni matokeo ya miezi ya mafunzo, majaribio na ubunifu wa wanafunzi wa kozi maalum za Klabu ya Sanaa ya AI, na unalenga kusimulia dhana za nuru za Qur’ani Tukufu kwa lugha mpya ya kisanaa na kiteknolojia.

Wageni hukutana na mitindo mbalimbali, mbinu na maelezo ya kimaono; kuanzia tafsiri za kisanaa za ubunifu hadi simulizi sahihi na za utafiti, zote zikitengenezwa kwa msaada wa zana za AI na mwongozo wa wataalamu.

Maonyesho haya ya pili ya kazi za Qur’ani Tukufu kwa teknolojia ya AI yanapokea wapenda sanaa, wasanii, watafiti na wanaharakati wa teknolojia kuanzia Jumamosi hadi Jumanne, kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni.

Habari zinazohusiana
captcha