IQNA

AI yatumika Makka kutoa mafunzo ya Qur’an kwa lugha 10

20:45 - March 05, 2025
Habari ID: 3480310
IQNA – Jukwaa la masomo ya Qur;an linalotumia Akili Mnemba au AI limezinduliwa katika Msikiti Mkuu wa Makka.

Mradi uliopewa jina “Al-Maqraa”, unatoa elimu ya Qur’an kwa lugha 10 tofauti.

Rais wa Mambo ya Dini katika Msikiti Mkuu wa Makka yaani Masjid Al Haram na Msikiti wa Mtume au Al Masjid An Nabawi Sheikh Abdulrahman Al-Sudais alizindua programu hiyo, Shirika la Habari la Saudi (SPA) liliripoti Jumanne.

Sheikh Al-Sudais alisema kuwa Al-Maqraa ni jukwaa la kimataifa la elimu ya Qur’ani ambalo linachanganya usahihi, mbinu za kisasa, mbinu kali, na teknolojia ya AI.

“Uzinduzi huu ni zawadi ya Ramadhani kutoka kwa Ufalme wa Saudi Arabia kwa Waislamu wote na wageni wa Msikiti Mkuu wa Mecca,” alisema.

Al-Maqraa inatoa programu kamili ya kusoma Qur’ani, Tajweed, na kuhifadhi, chini ya uangalizi wa walimu wenye sifa.

Inajumuisha mfumo wa usimamizi unaoambatana na Sharia ili kufuatilia utendaji katika duara za masomo ya Qur’ani, ripoti za kina za uchambuzi, mazingira ya kielimu yanayohamasisha, usajili rahisi katika duara za masomo, na mfumo kamili wa utoaji wa vyeti vya usomaji wa Qur’ani vinavyotambulika.

Mradi huu unalenga kukuza maadili ya Kiislamu miongoni mwa wanafunzi wanaohifadhi Qur’ani katika Msikiti Mkuu huku ukitoa mazingira rahisi ya kujifunza.

Jukwaa la Al-Maqraa, moja ya mipango muhimu ya utajiri ya urais, linaakisi mafundisho ya Mtume: “Bora miongoni mwenu (Waislamu) ni wale wanaojifunza Qur’ani na kuwafundisha wengine.”

3492167

Kishikizo: akili qurani tukufu
captcha