IQNA

Umrah

Zaidi ya Waumini 360,000 wametembelea Al Rawda Al Sharifa katika Msikiti wa Mtume kwa Wiki Moja

21:08 - January 04, 2025
Habari ID: 3480003
IQNA – Al Rawda Al Sharifa katika Al Masjid An Nabawi yaani Msikiti wa Mtume  mjini Medina ilitembelewa na zaidi ya waumini 367,000 wiki iliyopita.

Msikiti wa Mtume, eneo la pili takatifu zaidi katika Uislamu, ulipokea waumini na wageni milioni 5.6 wiki iliyopita huku huduma zikiendelea bila shida, kulingana na takwimu kutoka kwa shirika la serikali linalosimamia eneo hilo.

Mamlaka ya Jumla ya Huduma za Msikiti wa Mtume ilisema idadi hiyo ilijumuisha waumini 367,729 waliotembelea na kusali katika Al Rawda Al Sharifa lilipo kaburi la Mtume Mohammed (SAW)  ndani ya msikiti huo mtakatifu.

Ziara hizo zilifanywa kwa kuzingatia kanuni za usimamizi wa umati na ratiba tofauti zilizowekwa kwa wanawake na wanaume.

Mamlaka za Saudi Arabia zimekuwa zikisisitiza mara kwa mara kwamba wageni wa Al Rawda Al Sharifa lazima wachukue zami kwa njia ya kielektroniki au kiintaneti kabla ya kufika eneo hilo, na kufika kulingana na miadi iliyowekwa ili kuepusha msongamano.

Wiki iliyopita, waumini wasiopungua 46,731 wasiozungumza Kiarabu walinufaika na huduma za mawasiliano kwa lugha nyingi zinazopatikana ndani ya msikiti, kulingana na takwimu.

Wakati huo huo, kazi za kusafisha na kuua vijidudu zilifanywa kwa kutumia lita 24,256 za dawa za kusafisha. Aidha, tani 1,460 za maji ya Zamzam zilitolewa kwa waumini msikitini kote na milo 179,056 ya kufuturu (Iftar) ilisambazwa katika maeneo yaliyotengwa.

Baada ya kufanya Umrah au Hija ndogo katika Msikiti Mkuu, eneo takatifu zaidi la Uislamu huko Makka , Mahujaji wengi huenda Medina kusali katika Msikiti wa Mtume na kutembelea alama nyingine za Kiislamu katika jiji hilo.

Zaidi ya Waislamu milioni 280 walisali msikitini humo mwaka 2023.

3491315

Habari zinazohusiana
captcha