IQNA

Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu

Maandalizi yanaendelea kwa Mashindano ya 41 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran

22:14 - January 20, 2025
Habari ID: 3480082
IQNA – Kamati ya maandalizi ya Mashindano ya 41 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaendelea na maandalizi kwa ajili ya mashindano hayo, afisa mmoja alisema.

Jafar Hosseini, mkuu wa Mambo ya Qur'ani katika Idara ya Wakfu na Mambo ya Hisani ya mkoa wa Khorasan Razavi, alibainisha kwamba mashindano hayo hufanyika kila mwaka kabla ya siku yenye baraka ya Mab’ath (uteuzi wa kuwa nabii) ya Mtume Mtukufu Muhammad Al Mustafa (SAW).

Mwaka huu pia, yataanza mkesha Mab’ath katika ukumbi wa Quds wa kaburi (Haram) takatifu la Imam Ridha (AS) huko Mashhad tarehe 26 Januari, alisema.

Hosseini alibainisha kuwa hafla ya kufunga itafanyika tarehe 31 Januari, ambapo washindi katika kategoria za usomaji Qur'ani, kuhifadhi na Tarteel kwa wanaume na wanawake watatajwa na kupewa tuzo.

Akiyafafanua kama moja ya matukio muhimu zaidi ya Qur'ani kwenye kiwango cha kimataifa, alisema mashindano hayo yamepokewa kwa hamasa kubwa kutoka kwa wasomaji na wahifadhi wa Qur'ani kutoka kote ulimwenguni.

Hadi sasa, mikutano kadhaa imefanyika na kamati ya maandalizi ili kuhakikisha kuwa toleo hili la mashindano linakuwa kubwa zaidi iwezekanavyo, na mikutano hii bado inaendelea, aliendelea kusema.

Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran huandaliwa kila mwaka na Shirika la Wakfu na Mambo ya Hisani la nchi.

Yanalenga kukuza utamaduni na maadili ya Qur'ani miongoni mwa Waislamu na kuonyesha vipaji vya wasomaji na wahifadhi wa Qur'ani.

3491513

Habari zinazohusiana
captcha