Hujjatul-Islam Mohammad Ahmadzadeh, mkurugenzi mkuu wa Idara ya Wakfu katika Mkoa wa Khorasan Razavi alitoa maoni hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari huko Mashhad Jumatatu.
Amesema ni heshima kuwa mwenyeji wa duru ya mwisho ya mashindano hayo maarufu, ambayo ni tukio kubwa zaidi la Qur'ani la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, katika Haram Takatifu ya Imam Ridha (AS) huko Mashhad.
Amebainisha kuwa fainali zitahudhuriwa na wasomaji na wahifadhi wa Qur'ani 57 kutoka nchi 27.
Wamefika hatua hii kutoka kati ya karibu wanaharakati 400 wa Qur'ani kutoka nchi 104 ambao walishiriki katika raundi ya kwanza, aliongeza.
Afisa huyo pia alibainisha kuwa ili kufaidika zaidi na uwepo wa wasomi wa Qur'ani mjini humo, duru 41 za usomaji Qur'ani zitapangwa Mashhad wakati wa mashindano hayo.
Kuhusu matangazo ya vyombo vya habari ya mashindano hayo, alisema mitandao yote nchini itaakisi tukio hilo, ambapo Televisheni ya Qura'ani ya Iran, Quran TV, itakuwa kituo kikuu na cha kwanza kwa matangazo ya moja kwa moja ya shindano hilo.
Mashindano hayo pia yataakisihwa katika mitandao ya redio na televisheni 170 kupitia Muungano wa Vituo vya Redio na Televisheni vya Kiislamu , Hujjatul Islam Ahmadzadeh alisema.
Alibainisha pia kuwa washiriki watakuwa na mkutano rasmi na Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyed Ali Khamenei jijini Tehran.
Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran huandaliwa kila mwaka na Shirika la Wakfu na Mambo ya Hisani
Lengo lake ni kukuza utamaduni na maadili ya Qur'ani miongoni mwa Waislamu na kuonyesha vipaji vya wasomaji na wahifadhi wa Qur'ani.
Raundi ya mwisho ya toleo la 41 inatarajiwa kufanyika Mashhad mnamo Januari 26-31, 2025.
3491539