IQNA

Dua za Kila Siku za Mwezi wa Ramadhani- Siku ya Sita

5:43 - March 07, 2025
Habari ID: 3480320
Dua hizi za kila siku za Mwezi wa Ramadhani husomwa toka mwanzo ya tarehe mosi Ramadhani hadi siku ya mwisho katika mwezi huu mtukufu. Kila dua ina siku yake, na inaweza kusomwa mara nyingi kadiri ya uwezo wa mtu mwenyewe.

Day 6 of Ramadan: Today’s Special Supplication

Ee Mwenyezi Mungu! Usinidhalilishe katika mwezi huu kama kilipizo cha kukuasi kwangu, na wala Usinipige katika mwezi huu kwa mjeledi wa maangamizo yako na Uniepushie mbali na mambo yote yawezayo kunitumbukiza katika hasira zako, (nakuomba Unitakabalie maombi yangu haya) kwa Ukarimu wako na Baraka zako Ewe Mwombwa.

captcha