Dua hizi za kila siku za Mwezi wa Ramadhani husomwa toka mwanzo ya tarehe mosi Ramadhani hadi siku ya mwisho katika mwezi huu mtukufu. Kila dua ina siku yake, na inaweza kusomwa mara nyingi kadiri ya uwezo wa mtu mwenyewe.

Ee Mwenyezi Mungu! Kujaalie kufunga kwangu katika mwezi huu kuwe ni kufunga kwa wanaofunga (Saumu zao zikawa sahihi na kukubaliwa. Na kusimama kwangu kwa ibada kuwe sawa na wanaofanya ibada (zao zikapokelewa), na Uniepushe na usingizi wa wavivu, niwezeshe niukamilishe Ewe Mola wa Walimwengu, na Uniafu Ewe Mwenye kuwasamehe wakosaji.