IQNA

Dua za Kila Siku za Mwezi wa Ramadhani- Siku ya 16

8:47 - March 17, 2025
Habari ID: 3480385
Dua hizi za kila siku za Mwezi wa Ramadhani husomwa toka mwanzo ya tarehe mosi Ramadhani hadi siku ya mwisho katika mwezi huu mtukufu. Kila dua ina siku yake, na inaweza kusomwa mara nyingi kadiri ya uwezo wa mtu mwenyewe.

Day 16 of Ramadan: Today’s Special Supplication

Ee Mwenyezi Mungu! Niwafikie katika mwezi huu kwa kusikizana na watu wema, na Uniepushe katika mwezi huu kurafikiana na wabaya, Uniweke kwa Rehema yako kwenye Nyumba ya Utulivu kwa Utukufu wako Ee Bwana Mwabudiwa wa viumbe.

captcha