Ripoti zinasema kuwa, makumi ya Wazayuni mapema leo Jumatatu waliuhujumu Msikiti wa Al Aqsa kupitia lango la Al-Magharebah na kuuvunjia heshima huku askari wa utawala wa Israel waliwazuia Wapalestina kutekeleza ibada Msikitini hapo wakati wa hujuma hiyo.
Walowezi hao wa Kizayuni walitekeleza ibada za Kiyahudi katika uwanja wa Msikiti wa Al Aqsa kabla ya kuondoka wakipitia mlango wa Al Silsila.
Katika miaka ya hivi karibuni, utawala wa Kizayuni wa Israel umeshadidisha hujuma na uvamizi wake dhidi ya maeneo ya Wapalestina ukifanya njama za kufikia malengo yake haramu katika ardhi za Wapalestina.
Msikiti wa al-Aqsa ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu umekuwa ukiandamwa na njama mtawalia za utawala vamizi wa Israel, hatua ambazo zinakwenda sambamba na ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika maeneo ya Wapalestina.