IQNA

Sala ya Ijumaa

Maelfu Wanahudhuria Swala ya Ijumaa katika Msikiti wa Al-Aqsa

12:42 - July 09, 2022
Habari ID: 3475480
TEHRAN (IQNA) – Swala ya Ijumaa katika Msikiti wa Al-Aqswa huko al-Quds (Jerusalem) ilihudhuriwa na makumi ya maelfu ya waumini Wapalestina jana, ambayo iliadhimisha Siku ya Arafah.

Sala hiyo imesaliwa licha ya hatua kali zilizowekwa na utawala wa Kizayuni katika milango ya Mji Mkongwe wa Al-Quds unaokaliwa kwa mabavu.

Idara ya Wakfu ya al-Quds ilikadiria kuwa karibu waumini 50,000 waliswali Sala ya Ijumaa katika Siku ya Arafa katika kiwanja cha Al-Aqsa, wote wakitokea al-Quds, maeneo yaliyokaliwa kwa mabavu mwaka 1948 na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Shirika la Habari la Palestina, Wafa, liliripoti kuwa vikosi vya utawala ghasibu wa Israel vilivyowekwa karibu na Al-Aqsa, viliwazuia waumini na kuangalia vitambulisho vyao, na kuwazuia makumi ya watu kuingia msikitini, huku wakiwaruhusu makumi ya walowezi kufanya ibada za  Kiyahudi za Talmudi mbele ya Msikiti huo katika Lango la Simba, moja ya milango ya Msikiti wa Al-Aqsa.

Msikiti wa Al Aqsa umegeuzwa kuwa eneo la kutamba na kujifaragua askari wa utawala haramu wa Israel na walowezi wa Kizayuni wanaochukua hatua zinazolenga kuubadilisha utambulisho wa Kiislamu na Kikristo wa mji wa al-Quds na badala yake kuufanya kuwa na nembo za Uzayuni.

Mji wa Quds ulipo msikiti wa Al Aqsa ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu ni sehemu isiyotenganika na ardhi ya Palestina na moja ya maeneo matatu muhimu zaidi matakatifu ya Kiislamu.

3479625

 

captcha