IQNA

Wenye kupinga Uislamu Denmark watozwa faini kwa kuvunjia heshima nakala ya Qur'ani

20:26 - May 17, 2025
Habari ID: 3480696
IQNA– Wanaume wawili wamepatikana na atia ya kuvunjia heshima nakala ya Qur'ani Tukufu na kila mmoja kutozwa faini ya kroner za Denmark 10,000 (sawa na dola 1,500) huko Denmark.

Mahakama ya Denmark Ijumaa iliwaadhibu hawa wawili kwa kosa la kuvunjia heshima nakala ya Qur'ani Tukufu, miongoni mwao kinara wa chama kinachopinga Uislamu.

Wanaume hao walionekana kuvunja sheria inayozuia “kuvunjia heshima maandiko ya kidini,” ambayo ilianza kutumika Desemba 2023.

Sheria hii ilitungwa baada ya maandamano yaliyofuatia matukio ya kuvunjia heshima nakala ya Qur'ani Tukufu  Denmark na Uswidi, yaliyosababisha hasira kubwa katika nchi kadhaa za Kiislamu.

Kwa mujibu wa hukumu, mmoja wa wanaume hao, aliyezaliwa mwaka 1988, akirarua kurasa za nakala ya Qur'ani Tukufu iliyofasiriwa kwa Kiingereza kisha akaacha kitabu hicho kitukufu kwenye bwawa la maji.

Tukio hilo lilirushwa moja kwa moja katika ukurasa wa Facebook wa chama cha kupinga Uislamu, Stram Kurs, kinachoongozwa na Rasmus Paludan, ambaye pia ametozwa faini.

Paludan alitangaza kwamba amepinga hukumu hiyo.

Mahakama ilibaini kwamba washtakiwa walifanya vitendo hivyo “pamoja,” kama ilivyoelezwa katika hukumu yake.

Sheria za Denmark zinakataza kwa wazi kuchoma, kudhuru, kurarua kurasa au kupiga teke, nk maandiko ya dini.

3493110

Habari zinazohusiana
captcha