IQNA

Kongamano kubwa la Qur'ani Tukufu lafanyika Tanga, Tanzania

15:35 - May 25, 2025
Habari ID: 3480738
IQNA-Kongamano kubwa na la aina yake la Qur'ani Tukufu imefanyika katika mji wa pwani wa Tanga nchini Tanzania na kuwavutia hadhirina kutokana na usomaji wa kipekee wa Tajweed na wa kupendeza.

Miongoni mwa wasomaji maarufu wa Qur'ani walioshiriki katika hafla hiyo iliyofanyika katika Mkwakwani ni Hamed Shakernejad na Ahmad Abolghasemi kutoka Iran na maqari wawili mashuhuri wa Tanzania ambao Rajai Ayoub na Iddi Shaaban.

Kongamano hilo linafanywa kwa ushirikiano wa Chuo Kikuu Jamiat al-Mustafa (s) tawi la Tanzania chini ya uongozi wa Hujjatul Islam wal Muslimin, Dr. Ali Taqavi, Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT) ikiongozwa na Mwenyekiti wake Taifa, Sheikh Dr. Alhad Mussa Salum, Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) likiwa chini ya Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Dr. Abubakar Zubair bin Ally, pamoja na Kitengo cha Utamaduni wa Iran kinachoongozwa na Dr. Maarifi.

Hili ni Kongamano la pili, na leo Jumapili Kongamano la tatu litafanyika Viwanja vya  Mnazi Mmoja, jijini Dar es salaam.

 

.

 

  • Mji wa Tanga wazizima - Qur'an
  • Mji wa Tanga wazizima - Qur'an
  • Mji wa Tanga wazizima - Qur'an
  • Mji wa Tanga wazizima - Qur'an
  • Mji wa Tanga wazizima - Qur'an
  • Mji wa Tanga wazizima - Qur'an
  • Mji wa Tanga wazizima - Qur'an
  • Mji wa Tanga wazizima - Qur'an
  • Mji wa Tanga wazizima - Qur'an
  • 4284370
Kishikizo: tanzania qurani tukufu
captcha