IQNA

Mfasiri: Ujumbe wa Qur’aniUna usambazwe kimataifa: Kiongozi wa Kidini

18:41 - May 30, 2025
Habari ID: 3480759
IQNA: Qur’ani Tukufu ina maarifa ya kimataifa yanayopaswa kufafanuliwa, na ujumbe wake unapaswa kuwasilishwa kwa ulimwengu mzima, amesema Hujjatul Islam Mohsen Qara’ati, mwanazuoni wa Kiislamu na mtafsiri wa Qur’ani kutoka Iran.

Akizungumza katika mkutano wa wakuu wa Wakfu wa Hazrat Mahdi (AS)  huko Jamkaran, Qom,nchini Iran Alhamisi, Hujjatul Islam Qara’ati alieleza kuwa Qur’ani ni kitabu cha maisha, akisisitiza kuwa mafundisho yake yanapaswa kuwa sehemu ya maisha ya watu.

Aidha, aliangazia umuhimu wa kumtambulisha Ahl-ul-Bayt (AS), hususan Imam Mahdi (AS) kwa jamii nzima, akisema kuwa ni wajibu wa viongozi wa taasisi hiyo kote nchini kufafanua hadhi na nafasi ya Imam Zaman (AS).

Hujjatul Islam Qara’ati aliongeza kuwa taasisi za kidini, vyuo vikuu na wizara ya elimu zina mchango mkubwa katika kueneza utamaduni wa Mahdism (kusubiri Mwokozi).

Hujjatul Islam Qara’ati ni mwandishi wa Tafsiri Nur, tafsiri ya Qur’ani Tukufu iliyoandikwa kwa lugha rahisi na inayoweza kueleweka na kila msomaji. Tafsiri hiyo ni ya aya zote za Qur’ani na imetoa ujumbe mfupi wa kiutendaji kutoka katika aya tukufu. Hivi karibuni kulizunduliwa tarjuma ya Tafsiri ya Nur katika hafla iliyofanyika nchini Tanzania.

3493271

 

captcha