Tafsiri hii mpya iliyotafsiriwa (Tarjumiwa) kwa Lugha ya Kiswahili, inayojulikana kwa jina "Tafsiri Nur", imeandikwa na: Hujjatul-Islam wal-Muslimin Muhsin Qiraati, na lugha yake ya awali ni Kiajemi. Sasa, Tafsiri hiyo sasa imetayarishwa kwa lugha fasaha ya Kiswahili baada ya kutarjumiwa kwa ufanisi mkubwa na Sheikh Dr. Baqir Matega, shirika la Abna limeripoti.
Uzinduzi huu, uliofanyika tarehe 20 Mei 2025, unachukuliwa kuwa hatua muhimu katika kusambaza maarifa ya Qur’an kwa wasemaji wa Kiswahili, na unalenga kuwapa waumini wa Kiislamu uelewa mpana na wa kina wa mafundisho ya Kitabu hiki Kitukufu kwa lugha wanayoifahamu vizuri.