Hayo yamesemwa na Mhandisi Ghazi Al-Shahrani, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka Kuu ya Masuala ya Msikiti Mtakatifu wa Makka na Msikiti wa Mtume mjini Madina.
Al-Shahrani amebaini kuwa watu 16,558,241 walitekeleza ibada ya Umra, huku Msikiti Mkuu wa Makka ukipokea jumla ya waumini 92,132,169 waliofika hapo kuswali. Wakati huo huo, Msikiti wa Mtume huko Madina ulipokea waumini 30,154,543 katika kipindi hicho.
Ramadhani huchukuliwa kuwa wakati maalum sana kwa Waislamu kutekeleza Umra – hija isiyo ya lazima – kutokana na thawabu zake za kiroho. Kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu, ibada zinazofanywa katika mwezi huu mtukufu huleta baraka nyingi zaidi, na hivyo kuufanya kuwa muda bora wa kutembelea misikiti mitakatifu.
Mbali na kutafuta kujitakasa kiroho, mahujaji wengi huchagua mwezi wa Ramadhani kwa ajili ya Umra ili kushiriki swala maalum, kufanya itikafu, na kunufaika mazingira ya ibada na unyenyekevu katika miji mitakatifu.
3492531