IQNA

Milo Milioni 17 ya Futari katika Misikiti ya Makka na Madina katika wiki Tatu za Ramadhani

11:06 - March 27, 2025
Habari ID: 3480448
IQNA – Zaidi ya milo milioni 17 ya Futari au Iftar imesambazwa katika Msikiti Mkuu wa Makka (Masjid al Haram)  na Msikiti wa Mtume Madina (Al Masjid an Nabawi) katika wiki tatu za kwanza za mwezi mtukufu wa Ramadhani mwaka huu.. 

Mamlaka ya Jumla ya Utunzaji wa Masjid Al Haram na Al Masjid An Nabawi ilitangaza kuwa imesambaza milo wa futari ipatayo 17,020,216 miongoni mwa waumini katika Misikiti Miwili Mitakatifu ndani ya siku 21 za kwanza za Ramadhani. 

Jambo hilo limewezekana kwa kushirikiana na mashirika mbalimbali ya misaada. 

Aidha, pakiti 17,190,000 za tende zilisambazwa kama sehemu ya juhudi za mamlaka kuwahudumia waumini, ikiwa ni pamoja na utoaji endelevu wa maji ya Zamzam. 

Katika kipindi hiki, mita za ujazo 27,105 za maji ya Zamzam zilitumika, sawa na takriban vikombe 150,614,000 au chupa 721,774. 

Mamlaka ilisisitiza kujitolea kwake katika kudumisha usafi wa Misikiti Miwili Mitakatifu wakati wote ili kuhakikisha mazingira salama na yenye afya, na kuondoa tani 4,529 za taka ndani ya kipindi hicho.

Katika mwezi mtukufu wa Ramadhani idadi kubwa ya waumini hufika katika maeneo hayo mawili matakatifu kwa ajili ya ibada na pia kwa ajili ya Umrah au Hija ndogo.

3492502

Habari zinazohusiana
captcha