IQNA

Israel imeua zaidi wafanyakazi 1,300 wa sekta ya elimu katika mauaji ya kimbari Gaza

15:09 - January 20, 2026
Habari ID: 3481824
IQNA-Ripoti ya pamoja ya Wizara ya Elimu na Elimu ya Juu ya Palestina imeripoti kuwa, kuanzia Oktoba 2023 hadi Oktoba 2025, walimu wasipungua 1,377 na wafanyakazi wa elimu waliuawa shahidi na 4,757 wamejeruhiwa katika mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na utawala dhalimu wa Israel huko Gaza.

Katika kipindi hicho hicho, zaidi ya wanafunzi 20,000 wa Kipalestina waliuawa shahidi na wengine 31,000 walijeruhiwa.

Ripoti ya pamoja ya Wizara ya Elimu na Elimu ya Juu ya Palestina inasema, mfumo wa elimu wa Gaza umelengwa na uharibifu uliopangwa na utawala wa Kizayuni wa Israel, na kitendo hiki ni kielelezo cha mauaji ya kimbari.

Habari inayohusiana:

Ripoti hiyo inasema, kutokana na uharibifu wa makusudi wa miundombinu ya elimu uliofanywa na Israel huko Gaza, sasa shule na vyuo vikuu vimegeukia elimu ya mtandaoni.

Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) pia limeripoti kwamba watoto 658,000 wa Ukaknda wa Gaza wamenyimwa elimu katika miaka miwili iliyopita.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Afya ya Palestina imeeleza katika takwimu zake za hivi karibuni kwamba, Wapalestina zaidi ya 71,000 wameuawa shahidi katika vita vya mauaji ya kimbari vilivyoanzishwa na utawala wa kizayuni wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza, Oktoba 2023.

3496119

Habari zinazohusiana
captcha