Wizara ya Afya ya Palestina huko Gaza imeripoti kuwa, idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na mashambulizi yanayoendelea ya utawala ghasibu katika Ukanda wa Gaza imeongezeka na kufikia 56,077, huku watu 129,880 wakijeruhiwa tangu kuanza kwa vita tarehe 7 Oktoba 2023.
Kwa mujibu wa taarifa mpya za kila siku za wizara hiyo, watu 144 waliuawa katika muda wa saa 24 zilizopita, wakiwemo wanne ambao miili yao iliopolewa kutoka chini ya vifusi, na wengine 560 walijeruhiwa na kufikishwa hospitalini.
Waathiriwa wengi bado wanaaminika kuwa wamenaswa chini ya vifusi au wamelala barabarani, lakini mashambulizi ya mabomu yanayoendelea yamezuia wafanyakazi wa dharura kuwafikia.
Duru za kimatibabu huko Gaza pia zimethibitisha kuwa Wapalestina 19 waliuawa katika mashambulizi ya anga ya Israel mapema Jumatano katika maeneo mengi ya Ukanda huo.
Miongoni mwa waliofariki ni watu sita waliokuwa wakisubiri karibu na vituo vya kusambaza misaada kwa ajili ya chakula.
Hii inaleta jumla ya idadi ya wale maafisa wa afya wanawaita "Breadline Martyrs" - watu waliouawa wakati wakitafuta msaada wa kibinadamu - hadi 473, na angalau wengine 3,602 walijeruhiwa katika mashambulizi sawa ya uhalifu.
Tangu awamu ya hivi majuzi zaidi ya mashambulizi ya Israel kuanza Machi 18, 2025, Wapalestina wasiopungua 5,334 wameuawa na 17,839 kujeruhiwa.
Zaidi ya watu 10,000 bado wanaripotiwa kutoweka na wanaaminika wamenasa chini ya vifusi au hawajulikani waliko kote Gaza.
4290737