
Timothy McCord, kupitia makala iliyochapishwa katika tovuti diem25.org, aliandika: Katika Siku ya Watoto Duniani, UNICEF inatuita “kuimarisha sauti za watoto na kusimama kwa ajili ya haki za kila mtoto.”
Hata hivyo, Israel, ambayo iliridhia mkataba huu mwaka 1991, imegeuka kuwa dola dhalimu inayowalenga watoto wa Palestina kwa makusudi.
Mnamo Septemba mwaka huu, Save the Children ilitangaza kuwa katika kipindi cha takriban miezi 23 tangu Oktoba 7, 2023, zaidi ya watoto 20,000 wameuawa katika mashambulizi ya Israel dhidi Gaza. Takribani 1,009 walikuwa chini ya mwaka mmoja , 450 kati yao walizaliwa na kuuawa ndani ya kipindi cha mauaji haya. Katika miezi minne ya mwanzo, idadi ya vifo vya watoto Gaza ilizidi jumla ya vifo vya watoto katika vita vya dunia kwa miaka minne.
Ripoti ya Global Protection Cluster ilionyesha kuwa kufikia Julai 3, 2025, zaidi ya watoto 40,500 wamejeruhiwa; wastani wa watoto 15 kwa siku hupata ulemavu wa kudumu, na watoto 10 kwa siku hupoteza mguu mmoja au yote mawili.
Mnamo Januari 2025, UNICEF ilitangaza kuwa “Ukanda wa Gaza sasa una idadi kubwa zaidi ya watoto waliokatwa viungo kwa uwiano wa idadi ya watu kuliko sehemu yoyote duniani.”
Uchunguzi wa gazeti la Kiholanzi de Volkskrant mnamo Septemba 2025 ulibaini kuwa madaktari wa kimataifa waliokuwa wakihudumu Gaza waliona mpangilio wa kutisha: watoto wakiwa na jeraha moja la risasi kichwani au kifuani, ishara ya kulengwa kwa makusudi. Madaktari 15 wa kimataifa walishuhudia kesi 114 za watoto wenye umri wa miaka 15 na chini, wengi wao wakifariki. Kamanda wa zamani wa jeshi la Uholanzi, Mart de Kruif, alisisitiza: “Iwapo unaona idadi kubwa ya risasi kifuani na kichwani, hilo si kosa la vita , ni kulenga kwa makusudi.”
Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Mtoto ilisema wazi kuwa “vitendo vinavyoendelea vya Israel ni ukiukaji wa moja kwa moja vinavyopiga moyo wa haki zilizowekwa katika Mkataba wa Haki za Mtoto.”
Israel inalazimika kulazimishwa na mataifa kusitisha mauaji ya halaiki, uvamizi haramu, mfumo wa ubaguzi na dhulma dhidi ya Wapalestina, na kutekeleza kikamilifu mkataba huo. Haki ya kimsingi ya watu wa Palestina ya kujitawala haiwezi tena kunyimwa.
Watoto wa Palestina wameuawa, kujeruhiwa, kunyimwa chakula, kuathirika kisaikolojia, kufungwa bila kesi, kudhalilishwa na kuteswa, huku dunia ikiendelea kukosa kuchukua hatua madhubuti za kukomesha maafa haya. Mataifa lazima yakomeshe ukimya na ushirikiano wao ulioendeleza hali hii kwa muda mrefu mno.
Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Mataifa, Francesca Albanese, katika ripoti yake “Gaza Genocide: a collective crime” alichambua kwa kina ushirikiano huu na kueleza wazi hatua zinazopaswa kuchukuliwa na mataifa. Hakuna udhuru wa kutokutekeleza.
Kwa ajili ya watoto wa Palestina na kwa ajili ya ubinadamu, mataifa hayapaswi kuchelewa tena. Chukueni hatua sasa!
3495472