Hayo yamesemwa katika Duru ya Tisa ya Kongamano la Kimataifa la Haki za Binadamu la Marekani kwa Mtazamo wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu likiangazia Operesheni ya Ahadi ya Kweli, Sayed Hassan Nasrallah.
Washiriki wa mkutano huo walisikitishwa na vita vya mauaji ya kimbari vinavyoendelezwa na utawala wa Israel dhidi ya Wapalestina kwa uungaji mkono wa nchi za Magharibi kwa hilo.
Nasser Abu Sharif, mwakilishi wa Harakati ya Jihad ya Kiislamu ya Palestina mjini Tehran amesema katika hotuba yake kwamba Marekani inatoa uungaji mkono wa kila namna kwa utawala wa Kizayuni na hivyo kuusaidia kutenda jinai.
Msaada wa Marekani haukomei kwa kusambaza silaha lakini pia unajumuisha aina nyingine za usaidizi wa kisiasa, alisema.
Israel kamwe haiadhibiwi kwa uhalifu wake kwani nchi za Magharibi zimepitisha misimamo miwili kuhusu suala la Palestina, alisema, akiongeza kuwa haki inapaswa kuwa kwa wote, wakiwemo Wapalestina.
Abu Sharif aliendelea kusema utawala wa Israel, kwa uungaji mkono kwa Marekani, umeendeleza vita vyake vya kigaidi hadi kusini mwa Lebanon na iwapo jumuiya ya kimataifa haitaukomesha, utawala huo utaendelea kufanya jinai.
Sheikh Ghazi Yusuf Hunaina, mwenyekiti wa bodi ya wadhamini wa Jumuiya ya Maulamaa wa Kiislamu Lebanon, alikuwa mzungumzaji mwingine katika mkutano huo.
Alifafanua juu ya vipengele tofauti vya tabia ya Katibu Mkuu wa Hizbullah Sayed Hassan Nasrallah, akisema kiongozi huyo aliyeuawa shahidi wa harakati ya upinzani alijitahidi kuleta umoja kati ya Waislamu wa Shia na Sunni.
Amesema Nasrallah alikuwa na maingiliano mazuri na wanazuoni wa Shia na Sunni katika Jumuiya ya Maulamaa wa Kiislamu wa Lebanon na pia alifanya juhudi za kuwaunganisha Waislamu na Wakristo nchini humo kwa sababu silaha kuu katika kukabiliana na adui ni kudumisha umoja.
Katika maelezo yake Sheikh Hunaina amesema viongozi wa muqawama au mapambano ya Kiislamu huko Iraq, Lebanon, Yemen, Syria, Palestina na Iran wanasisitiza ukweli kwamba, njia bora ya kusonga mbele ni kupambana kwa silaha na utawala wa Kizayuni hadi usitishe kampeni yake ya mauaji ya kimbari na ukatili.
4241468