IQNA

Marekani yakosolewa kwa kumruhusu katili Netanyahu kuhutubia Kongresi

15:48 - July 25, 2024
Habari ID: 3479180
IQNA-Kongresi ya Marekani imekosolewa sana kwa kumpa Waziri Mkuu wa Israel, katili Benjamin Netanyahu, jukwaa la kuhutubia wawakilishi na maseneta wa nchi hiyo licha ya kiongozi huyo kutambuliwa kuwa ni mhalifu wa kivita na mtenda jinai dhidi ya binanadamu kutokana na mauaji ya kimbari yanayoendelea huko Gaza.

Maelfu ya watu waliingia katika mitaa ya Washington, DC jana kupinga hotuba ya Benjamin Netanyahu.

Usalama uliimarishwa kabla ya hotuba ya nne ya Netanyahu kwa wabunge wa Marekani na sehemu kubwa ya eneo la Capitol ilifungwa kwa umma.

Lakini hakuna kilichowazuia watu kupinga sera za Netanyahu katika Ukanda wa Gaza na kutaka kusitishwa kwa mapigano katika eneo hilo lililozingirwa.

Wakipeperusha bendera za Palestina, waandamanaji waliimba "Palestine Huru" na "Sitisha mapigano sasa." Pia walishikilia mabango yaliyosema "Mkamateni Netanyahu," "Simama na Palestina! Maliza Kazi Sasa!" na “Mauaji ya Kimbari ni Mstari Wetu Mwekundu.”

Naye Katibu Mkuu wa Mpango wa Kitaifa wa Palestina, Mustafa Barghouti, amesema kilichotokea jana ni "kikao cha aibu kwa Bunge la Merekani kwa kumpa ukumbi mhalifu wa kivita Netanyahu, ambaye anafanya uhalifu wa mauaji ya halaiki, mauaji ya kimbari na kuwatesa Wapalestina kwa njaa."

Mustafa Barghouti ameongeza kuwa, "Ustaarabu uliozungumziwa na Netanyahu sio ustaarabu, bali ni mproromoko. Netanyahu ameua Wapalestina 48,000 huko Gaza wakiwemo watoto 17,000, amekata mikono na miguu ya watoto 1,200 wa Kipalestina, na kuwalazimisha Wapalestina milioni mbili kuwa wakimbizi baada ya kubomoa makazi yao."

Kuhusu hotuba ya Waziri Mkuu wa Israel katika Kongresi ya Marekani, Seneta wa kujitegemea wa Marekani, Bernie Sanders, amesema kuwa Netanyahu "sio tu mhalifu wa vita, bali pia kidhabi na muongo." 

Kabla ya hapo, seneta huyo wa Vermont alikuwa amesema kuwa: "Hii inakuwa mara ya kwanza katika historia ya Marekani kwa mhalifu wa kivita kupewa heshima hiyo."

Kwa upande wake, Spika wa zamani wa Kongresi ya Marekani, Nancy Pelosi alisema kuwa hotuba ya Netanyahu ilikuwa "uwasilishaji mbaya zaidi kuwahi kutolewa na mgeni aliyepewa heshima ya kuhutubia Congress."

Harakati ya Jihad Islami ya Palestina imesema kwamba hotuba iliyotolewa na Netanyahu mbele ya Congress ilijaa uongo na kashfa, na kwamba amethibitisha katika hotuba yake kwamba utawala wake dhaifu unaendeleza uwepo wake kutokana na vita.

Taarifa ya Jihad Islami imeongeza kuwa: "Uongo wa Benjamin Netanyahu kwamba jeshi lake halijaua raia hata mmoja katika shambulio la Rafah ni dhihaka kwa ulimwengu," na imesisitiza kwamba hotuba yake inaonyesha wazi kwamba hana nia ya kumaliza uvamizi na mashambulizi yake dhidi ya Gaza. Imesema: Hotuba hiyo "imejaa uongo na haitafanikiwa kuficha kushindwa kwake kukabiliana na Muqawama au kuficha uhalifu wa kivita na mauaji ya kimbari yanayofanyika Gaza."

3489241

Habari zinazohusiana
Kishikizo: mauaji ya kimbari gaza
captcha