"Vita vya kikatili vya Israel huko Gaza vinajumuisha mashambulizi ya kiholela na yasiyo na uwiano, pamoja na hatua zinazozuia idadi ya watu kupokea misaada ya kibinadamu. Hii ni kinyume na sheria za vita," Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Espen Barth Eide alisema katika taarifa yake Jumamosi.
Utawala wa Israel bado kwa kiasi kikubwa inazuia upatikanaji wa chakula na misaada muhimu ya dharura, alisema. Umoja wa Mataifa ulionya kwamba bila kuongezeka kwa upatikanaji wa misaada ya kibinadamu na biashara ya chakula cha kibiashara, "Gaza itakabiliwa na njaa kamili ifikapo Novemba," Eide aliongeza.
“Raia, wagonjwa na majeruhi lazima wapate ulinzi, chakula na msaada muhimu wa kimatibabu,” alisisitiza waziri huyo.
Akisisitiza kwamba usitishaji vita, kuachiliwa kwa mateka hao, na misaada ya kutosha ya dharura kwa watu wa Ukanda wa Gaza ni hatua muhimu za kwanza, alisema usitishaji mapigano sio suluhu peke yake.
"Ni suluhisho la serikali mbili tu na heshima kwa sheria ya kimataifa linaloweza kutoa utulivu na usalama wa kudumu katika Mashariki ya Kati. Ninatoa wito kwa pande zote kuachana na mapigano ya silaha na badala yake kutumia diplomasia na mazungumzo," aliongeza waziri huyo.
Utawala wa Israel umeendelea na mashambulizi ya mauaji ya kimbari huko Gaza tangu Oktoba mwaka jana licha ya azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likitaka kusitishwa mara moja mapigano.
Takriban Wapalestina 42,200 wameuawa tangu wakati huo, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, na zaidi ya 98,300 wamejeruhiwa, kulingana na mamlaka ya afya ya eneo hilo.
Mashambulizi ya Israel yamewafanya takriban wakazi wote wa Ukanda wa Gaza kuwa wakimbizi kutokana na mzingiro unaoendelea ambao umesababisha uhaba mkubwa wa chakula, maji safi na dawa.
Israel inakabiliwa na kesi ya mauaji ya halaiki katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki kutokana na jinai zake huko Gaza.
3490247/