Katika tamko lililotolewa jioni ya Jumapili, Sheikh al-Tayeb aliwataka watu wote wenye dhamiri hai duniani kuchukua hatua za haraka kusitisha mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel huko Gaza, ambayo yameendelea kwa takriban miezi 22, na kuvunja mzingiro wa kikatili uliowekwa na utawala huo ghasibu dhidi ya Wapalestina, kwa mujibu wa ripoti ya Al-Quds Al-Arabi.
"Ubinadamu unapimwa," alisema kwa uchungu, "watoto na raia wasio na hatia wanauawa kinyama bila huruma, na wale wanaoendelea kuishi wanakufa kwa njaa, kiu, ukosefu wa maji safi na dawa, huku vituo vya afya vikiwa vimeacha kufanya kazi."
Sheikh al-Tayeb alilaani vikali njama ya wazi ya utawala wa Kizayuni kuwaua kwa njaa watu wa Gaza ambao ni wanyonge na wanaotafuta kipande tu cha mkate au tone la maji.
Aliongeza kuwa mashambulizi dhidi ya kambi za wakimbizi wa ndani na vituo vya usambazaji wa misaada ya kibinadamu kwa risasi za moto ni jinai kamili ya mauaji ya kimbari (genocide).
“Yeyote anayesaidia utawala huu wa Kizayuni kwa silaha, au kwa kauli za kinafiki au maamuzi yanayounga mkono, anashiriki kwa njia moja au nyingine katika jinai hii ya mauaji ya halaiki,” alisisitiza Sheikh huyo.
Mgogoro wa njaa katika Ukanda wa Gaza umefikia hali ya kutisha kutokana na kuimarishwa kwa mzingiro na utawala wa Kizayuni, ambao unazuia kuingia kwa aina yoyote ya misaada ya kibinadamu, akasema kwa majonzi.
3493962