IQNA

Iran yatekeleza operesheni za kulipiza kisasi dhidi ya Marekani na Israel

16:58 - March 02, 2026
Habari ID: 3482008
IQNA-Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC)  limetekeleza operesheni kadhaa za kulipiza kisasi hadi sasa kujibu uchokozi wa Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Katika operesheni hizo ambazo zimepewa jina la Ahadi ya Kweli 4, IRGC imetumia makombora na ndege zisizo na rubani kushambulia maeneo ya kijeshi ya  utawala haramu wa Israel na pia kambi za jeshi la kigaidi la Marekani katika nchi za eneo zikiwemo Qatar, UAE, Kuwait, Bahrain, Jordan, na Saudia. Iran imesisitiza kuwa haina vita na nchi hizo bali inalenga vituo vya jeshi la kigaidi la Marekani ambavyo vinahesabiwa kuwa ni ardhi ya Marekani katika nchi hizo za Kiarabu.

Marekani ilianzisha hujuma dhidi ya Iran Jumamosi Pamoja na kuwa kulikiwa kumefanyika mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja baina yake na Iran chini ya upatanishi wa Oman Alhamisi iliyopita jijini Geneva.  Awali Iran ilikuwa imeonya kuwa vita dhidi yake vitageuka na kuwa vita vya kieneo.

3496610

Kishikizo: irgc Ahadi ya Kweli
captcha