
Akizungumza na Televisheni ya Al Jazeera siku ya Jumapili, Abbas Aragchi amesema sheria za kimataifa zinapiga marufuku vikosi vya kigeni kumuua kiongozi yeyote wa nchi nyingine. Amesema mauaji hayo yanafanya vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran kuwa vikali na hatari zaidi.
Kufuatia shambulio la kikatili la utawala wa Kizayuni na Marekani, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Imam Sayyid Ali Khamenei aliuawa shahidi Jumamosi mchini akiwa katika ofisi yake Jumamosi asubuhi.
Kwingineko, Aragchi amesema Iran haina mipaka katika kujilinda na kuongoza kuwa operesheni za kijeshi za Iran zinafanyika katika fremu ya haki yake ya kisheria.
Aragchi amesiitiza kuwa uhusiano wa Iran na nchi Jirani za Ghuba ya Uajemi ni mzuri na kuongeza kuwa Iran haizilengi kijeshi nchi Jirani bali inalenga vituo vya kijeshi vya Marekani katika nchi hizo ambavyo vinatumiwa kuishambulia Iran.
Amesema sharti lolote la kumaliza vita ni Marekani na Israel kusitisha vita vya kichokozi na kutoa maelezo ya sababu ya uchokozi huo.
/3496612