
Vita hivyo vilianza tarehe 10 ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani Februari 28 kwa mashambulizi ya kigaidi ya Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Kwa mujibu wa taarifa, wananchi walifika uwanjani tangu kabla ya kuanza rasmi kwa hafla hiyo saa saba mchana, na idadi ya waliohudhuria iliendelea kuongezeka kila dakika ilivyopita. Kituo cha treni ya chini ya ardhi cha Enqelab kilijaa waumini na wananchi wanamapinduzi, ambapo kila treni ilileta makundi makubwa ya wakazi wa mji mkuu kuelekea mahali pa kuanzia safari ya mazishi.
Mashahidi wa hafla hii wanajumuisha makamanda wakuu wa kijeshi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambao walipoteza maisha katika siku ya kwanza ya Vita vya Ramadhani kufuatia shambulio lililofanywa na jeshi la kigaidi la Marekani na washirika wake wa Kizayuni.
Miili mitukufu ya mashahidi inapokelewa kwa heshima kuu. Mashahidi hao ni pamoja na:
Aidha wengine ambao mazishi yao yamefanyika Jumatano ni pamoja na makamanda wengine kadhaa wakiwemo Jenerali Darreh Baghi, Jenerali Ali Tajik, Jenerali Dawood Asgari, Jenerali Hosseini Motlaq, Jenerali Babaeian, Jenerali Helali na Jenerali Rezaeian. Halikadhalia pia yamefanyika katika hafla hiyo yamefanyika mazishi ya raia kadhaa ambao wameuawa shahidi vitani, wakiwemo watoto wadogo.
Mazishi hayo yamedhihirisha umoja wa kitaifa na imani thabiti ya wananchi wa Iran katika kutetea haki na utu wa Kiislamu.
Wakati wa kuanza kwa hafla hiyo, mifumo ya ulinzi wa anga ya Tehran ilianza kufanya kazi baada ya kuoenekana ndege za kivita za adui. Wananchi hawakutishika na walitoa kauli mbiu za “Allahu Akbar” na “Mauti kwa Marekani,” na “Mauti kwa Israel”
Katika hafla hiyo, wananchi walithibitisha tena utii wao kwa kiongozi wa tatu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei. Wakiwa wameinua mikono yao juu, walipaza sauti wakisema: “Ewe kiongozi mwadilifu na shujaa, tuko tayari, tuko tayari.”