
Kwa mujibu wa shirika la habari IQNA, Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah al‑Udhma Sayyid Ali Khamenei, alikuwa na mkutano wa kila mwaka na jamii ya Qur’ani nchini, sambamba na siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Video yenye kichwa ‘Maelezo ya mwisho ya kukutana kwa Kiongozi Shahidi na jamii ya Qur’ani’ imesambaa kwenye mitandao ya kijamii.
Picha hizi zinahusiana na siku ya kwanza ya mwezi wa Ramadhani mwaka 1447 Hijria, na zinaonyesha namna ya mapenzi, umakini, na uhusiano wa kina uliokuwepo kati ya Kiongozi Shahidi na maneno ya Wahyi.
Katika mkusanyiko huo, mazingira ya kiroho yaliyotokana na tilawa tukufu ya Qur’ani, pamoja na uwepo wa waqarii na wahudumu wa Qur’ani, yaliunda hali maalum yenye utulivu na kumbukumbu ya kudumu." Imam Khamenei aliuawa shahidi tarehe 10 ya mwezi mtukufu wa Ramadhani mwaka huu wa 1447 Hijria Qamaria katika hujuma ya kigaidi ya Marekani na utawala wa Israel.