waislamu - Ukurasa 71

IQNA

TEHRAN (IQNA) - Mwanazuoni wa ngazi za juu nchini Iran amesema migogoro katika nchi za Kiislamu inatokana na njama za madola ya kibeberu na pia Waislamu kupuuza maamurisho ya Qur'ani Tukufu kuhusu umoja.
Habari ID: 3471571    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/06/24

TEHRAN (IQNA)- Kongamano la 'Zawadi ya Mtume wa Rahma SAW' limepangwa kufanyika 30 Agosti mwaka huu kwa ushirikiano wa Baraza Kuu la Waislamu Uganda na Shirika la Utangazaji la Uganda, UBC.
Habari ID: 3471570    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/06/24

Katika kutetea timu ya taifa iliyosoma Al Fatiha kabla ya mechi
TEHRAN (IQNA)- Dhakir Lahidhab ni daktari mpasuaji ambaye Mtunisia ambaye katika kuwajibu wale waliokosoa hatua ya timu ya taifa ya soka ya nchi hiyo kusoma aya za Qur'ani kabla ya mechi na Uingereza katika Kombe la Dunia amesema binafsi husoma Qur'ani kabla ya kila oparesheni ya upasuaji.
Habari ID: 3471569    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/06/23

TEHRAN (IQNA)-Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu Jordan imetangaza mpango wa kuzindua vituo 50 vya kuhifadhi Qur'ani katika mkoa wa Karak nchini humo.
Habari ID: 3471568    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/06/22

TEHRAN (IQNA)- Wizara ya Elimu katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetangaza kuwa karibu wanafunzi milioni moja nchini wamehifadhi Qur’ani.
Habari ID: 3471566    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/06/20

TEHRAN (IQNA)- Golkipa wa Timu ya Taifa ya Soka ya Misri katika Kombe la Dunia la FIFA 2018 nchini Russia amekataa zawadi ya mchezaji bora ambayo alitunukiwa na shirika moja la utegenezaji na uuzaji pombe.
Habari ID: 3471565    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/06/19

TEHRAN (IQNA)- Hivi karibuni nchini Uingereza kumeanza kuuzwa wanaserere waliovishwa Hijabu maarufu kama "Salam Sisters" au "Madada wa Salam" ambao ni nembo ya mwanamke Muislamu anayeweza kuigwa.
Habari ID: 3471564    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/06/18

TEHRAN (IQNA)-Huku mvua za monsoon ziliendelea kunyesha katika kambi kubwa za wakimbizi Waislamu wa jamii ya Rohingya nchini Bangladesh, Umoja wa Mataifa umeonya kuwa maisha ya wakimbizi 200,000 yako hatarini.
Habari ID: 3471562    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/06/17

TEHRAN (IQNA)- Qarii wa Qur’ani kutoka Iran, Ustadh Ali Asghar Shoaei, ameibuka mshindi katika duru ya 11 ya Mashindano ya Qur’ani ya mubashara kupitia Televisheni ya Kimataifa ya Al Kawthar.
Habari ID: 3471561    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/06/16

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa: Tatizo la utawala wa Kizayuni wa Israel ni kuwa hauna uhalali, ni utawala ambao msingi wa uundwaji wake ni batili, kwa taufiki yake Mwenyezi Mungu na kwa hima ya mataifa ya Waislamu, utawala huo kwa yakini utaangamia."
Habari ID: 3471560    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/06/15

TEHRAN (IQNA)- Waislamu wawili wamethibitishwa kuuawa kwa kudungwa visu wakiwa msikitini katika wakiwa katika Itikaf, baada ya mtu mmoja kuvamia eneo hilo la ibada nchini Afrika Kusini.
Habari ID: 3471558    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/06/15

TEHRAN (IQNA) -Misikiti nchini Sweden ilishambuliwa mara 38 mwaka 2017, ikiwa ni ongezeko la mara 10 ya vitendo hivyo vya chuki dhidi ya Uislamu.
Habari ID: 3471557    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/06/14

TEHRAN (IQNA)- Waislamu zaidi ya milioni mbili walifurika katika Msikiti Mkuu wa Makka (al-Masjid al-Haram) na Msikiti wa Mtume SAW (al-Masjid an-Nabawi) mjini Madina Jumatatu.
Habari ID: 3471556    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/06/13

TEHRAN (IQNA)- Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) limelaani hatua ya ndege za kivita za Saudi Arabia kudondosha mabomu katika kituo kimoja cha afya cha kuwatibu watu wenye kipindupindu nchini Yemen ambacho kinasimamiwa na shirika hilo.
Habari ID: 3471555    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/06/13

TEHRAN (IQNA)- Wakuu wa utawala wa China wanawashikilia kwa nguvu Waislamu karibu milioni 1 katika kambi zenye msongamano mkubwa ambapo wanafunzwa kwa lazima itikadi za Kikomunisti.
Habari ID: 3471554    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/06/12

TEHRAN (IQNA)- Wakimbizi Waislamu wa jamii ya Rohingya ambao wamekimbia ukandamizaji katika ardhi zao za jadi nchini Myanmar wamebainisha masikitiko yao baada ya Umoja wa Mataifa kushindwa kuwatetea wapate haki ya uraia.
Habari ID: 3471552    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/06/11

Rais wa Uturuki atahadharisha
TEHRAN (IQNA) – Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki amemkosoa Kansela Sebastian Kurz wa Austria kufuatia uamuzi wa serikali yake kufunga misikiti saba na kuwatimua maimamu 40.
Habari ID: 3471550    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/06/10

TEHRAN (IQNA) - Jumatano iliyopita , Rais Donald Trump wa Marekani aliandaa katika Ikulu ya White House kile alichodai kuwa ni dhifa ya futari kwa ajili ya Waislamu, lakini la kushangaza ni kuwa Waislamu wa Marekani hawakualikwa.
Habari ID: 3471549    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/06/09

TEHRAN (IQNA)- Maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds (Jerusalem) yamefanyika leo kote duniani kwa lengo la kuunga mkono ukombozi wa Palestina na kulaani utawala ghasibu wa Israel.
Habari ID: 3471547    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/06/08

TEHRAN (IQNA)- Mshindi katika Mashindano ya Kuhifadhi Qur'ani ya eneo la Somaliland nchini Somalia ametunukiwa zawadi ya gari.
Habari ID: 3471542    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/06/03