iqna

IQNA

Waziri wa Mambo ya Ndani Pakistan
TEHRAN (IQNA)-Waziri wa Mambo ya Ndani Pakistan Ahsan Iqbal amesema Qur'ani Tukufu ni kama ramani ya njia katika mwaisha ya mwanadamu.
Habari ID: 3471374    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/01/28

TEHRAN (IQNA)-Waislamu zaidi ya 100,000 kutoka jamii ya Uighur nchini China wanasemekana kushikiliwa kwa nguvu katika kambi zenye msongamano mkubwa ambapo wanafunzwa itikadi za Kikomunisti.
Habari ID: 3471373    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/01/27

TEHRAN (IQNA)-Nakala nne nadra za Qur'ani Tukufu ni kati ya turathi zenye thamani katika maktaba ya Msikiti wa Sayyida Zainab mjini Cairo, Misri.
Habari ID: 3471372    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/01/26

TEHRAN (IQNA)-Arthur Wagner, mwanasiasa aliyekuwa chuki dhidi ya Uislamu amebadili msimamo ghafla na kutangaza kuwa amesilimu na hivyo kuukumbatia Uislamu katika maisha .
Habari ID: 3471370    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/01/24

TEHRAN (IQNA)-Waislamu nchini Marekani wamepanga kuswali mbele ya Ikulu White House mjini Washington DC na kisha kufanya maandamano makubwa ya kulalamikia ubaguzi wanaotendewa na utawala wa Rais Donald Trump.
Habari ID: 3471369    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/01/24

TEHRAN (IQNA)-Baraza la Waislamu Uingereza (MCB) limetangaza kuanzisha mpango mpya wa kukabiliana na ugaidi.
Habari ID: 3471366    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/01/22

TEHRAN (IQNA)-Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inapanga kuandaa mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya wanafunzi Waislamu katika mwezi wa Aprili sambamba na Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran.
Habari ID: 3471365    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/01/22

TEHRAN (IQNA)-Jumuiya ya Kimataifa ya Wanazuoni Waislamu (IUMS) imelaani tawala za Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kwa kuendelea kuwashikilia kinyume cha sheria wahubiri wa Uislamu.
Habari ID: 3471362    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/01/20

IQNA (TEHRAN)-Serikali ya Bangladesh inasema wakimbizi Waislamu Warohingya waliopata hifadhi nchini kufuatia ukatili wanaotendewa nchini Myanmar sasa wamefika milioni moja na idadi hiyo ni kubwa zaidi ya ile ambayo imekuwa ikitajwa katika vyombo vya habari.
Habari ID: 3471360    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/01/19

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA) Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema Marekani imekuwa ikifanya "ufidhuli mkubwa" kuhusu Quds Tukufu (Jerusalem) na kuongeza kuwa njama zake hizo hazitafika popote.
Habari ID: 3471357    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/01/17

TEHRAN (IQNA)-Mji wa Cape Town nchini Afrika Kusini unatekeleza sera za kuwavutia watalii wa tamaduni na dini mbali mbali na kwa msingi huo kuna mpango maalumu wa kuwavutia watalii Waislamu katika fremu ya Utalii Halali.
Habari ID: 3471356    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/01/16

TEHRAN (IQNA)-Hafidh wa Qur'ani Tukufu kutoka Morocco ametangazwa mshindi katika Mashindano ya Tisa ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu nchini Sudan na kutunukiwa zawadi yake Jumamosi usiku.
Habari ID: 3471355    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/01/15

TEHRAN (IQNA)-Nchini Canada, binti Muslamu mwenye umri wa miaka 11 ameshambuliwa na Hijabu yake kuraruliwa wakati akiwa njiani kuelekea shuleni katika tukio la hujuma ya chuki dhidi ya Waislamu.
Habari ID: 3471352    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/01/13

TEHRAN (IQNA)- Baraza la Mahusiano ya Kiislamu nchini Marekani (CAIR) lina mpango wa kutoa mafunzo maalumu ya njia za kukabiliana na vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu nchini humo.
Habari ID: 3471351    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/01/12

Inna Lillah wa Inna Ilayhi Rajioun
TEHRAN (IQNA)-Kiongozi wa Tariqa Muridiyyah (aṭ-Ṭariqat al-Muridiyyah) ya Senegal Sheikh (Serigne) Sidy Mokhtar Mbacke ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 94.
Habari ID: 3471350    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/01/11

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, ushahidi na nyaraka za kipelelezi zinaonesha kuwa machafuko ya hivi karibuni nchini Iran yalipangwa na pande tatu.
Habari ID: 3471349    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/01/10

TEHRAN (IQNA)-Jumuiya ya Kimataifa ya Vijana Waislamu imezawadia watu wa Djibouti nakala 15,000 za Qur’ani Tukufu.
Habari ID: 3471346    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/01/08

TEHRAN (IQNA)-Utawala wa Saudi Arabia unawazuia raia wa Qatar kutekeleza Ibada ya Umrah katika miji mitakatifu ya Makkah na Madinah.
Habari ID: 3471345    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/01/07

Khatibu wa Sala ya Ijumaa
TEHRAN- (IQNA) Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran amesema, fujo ambazo zimeshuhudiwa siku za hivi karibuni mjini Tehran zinaashiria kuwepo uchochezi wa Marekani na vibaraka wake.
Habari ID: 3471343    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/01/05

TEHRAN (IQNA)-Idadi ya Waislamu wanaoishi nchini Marekani inatazamiwa kuongezeka maradufu ifikapo mwaka 2050 na hivyo kuufanya Uislamu kuwa dini ya pili kwa ukubwa nchini humo.
Habari ID: 3471342    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/01/04