saudi arabia - Ukurasa 11

IQNA

TEHRAN (IQNA) Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Saudi Arabia zimetiliana saini mapatano kuhusu Ibada ya Hija katika mwa huu wa Hijria Qamaria.
Habari ID: 3472264    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/12/09

TEHRAN (IQNA) – Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen ametahadharisha hujuma ya muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia dhidi ya nchi hiyo na kusisitiza kuwa, amani haiwezi kurejeshwa nchini humo kupitia nguvu za kijeshi.
Habari ID: 3472193    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/10/29

TEHRAN (IQNA) - Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa taarifa baada ya kushambuliwa meli ya mafuta ya Iran karibu na bandari ya Jeddah, Saudi Arabia katika Bahari ya Shamu.
Habari ID: 3472167    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/10/11

Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon
TEHRAN (IQNA) - Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amekosoa msimamo wa baadhi ya nchi na asasi kuhusu shambulizi la ulipizaji kisasi la Jeshi la Yemen dhidi ya vituo vya kusafisha amfut aya petroli nchini Saudi Arabia na kusema, misimamo hiyo inaonyesha kuwa mafuta ya petroli yana thamani zaidi ya damu ya mwanadamu.
Habari ID: 3472141    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/09/21

TEHRAN (IQNA) – Rais Vladimir Putin wa Russia amenukulu aya kadhaa za Qur'ani Tukufu katika kutoa wito wa kumalizika vita dhidi ya Yemen ambavyo vilianzishwa miaka mitano iliyopita na muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia.
Habari ID: 3472133    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/09/17

TEHRAN (IQNA) – Mkuu wa Shirika la Hija na Ziara za Kidini Iran Ali Reza Rashidian amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imefanya mazungumzo na Saudi Arabia kuhusu Wairani kuanza tena kutekeleza Ibada ya Umrah.
Habari ID: 3472130    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/09/15

TEHRAN (IQNA) – Mchunguzi maalumu wa Umoja wa Mataifa ametangaza kuwa ushahidi unaonyesha mrithi wa ufalme wa Saudi Arabia na maafisa kadhaa wa ngazi ya juu wa ufalme huo walihusika na mauaji ya mwandishi habariJamal Khashoggi.
Habari ID: 3472008    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/06/20

TEHRAN (IQNA) - Vikosi vya Yemen vimetekeleza shambulizi jingine la ulipizaji kisasi kwa kuulenga uwanja wa ndege wa Abha, katika mkoa wa Asir kusini mwa Saudi Arabia. Shambulizi hilo limetekelezwa ikiwa ni katika kulipiza kisasi jinai dhidi ya Wayemen ambazo zimekuwa zikitekelezwa na Saudia na waitifaki wake katika kipindi cha miaka minne sasa.
Habari ID: 3472005    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/06/17

TEHRAN (IQNA)- Saudi Arabia inaendelea kulaaniwa kimataifa kw akuwanyonga raia wan chi hiyo kutokana na itikadi zao zinazokinzana na zile za watawala wa ukoo wa Aal Saud.
Habari ID: 3471928    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/04/24

TEHRAN (IQNA)- Mfalme Salman Bin Abdulaziz wa Saudi Arabia ameitembelea Bahrain katika safari fupi na kufanya mazungumzo na mfalme wa nchi hiyo Hamad bin Isa Aal Khalifa.
Habari ID: 3471898    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/04/04

TEHRAN (IQNA)- Kamati ya Bunge la Uingereza ambayo ilikuwa na jukumu la kuchunguza mauzo ya silaha za nchi hiyo mwaka 2017 imelaaniwa vikali kwa kupuuza uuzaji wa silaha kwa Saudi Arabia nchi ambayo inawaua raia kiholela katika vita vya Yemen.
Habari ID: 3471838    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/02/12

TEHRAN (IQNA)- Morocco imejiondoa katika muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia katika vita dhidi ya Yemen.
Habari ID: 3471836    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/02/10

Inna Lillah wa Inna Ilayhi Rajioun
TEHRAN (IQNA)-Mtu mwenye chuki za kimadhehebu amemuua mtoto aliyekuwa na umri wa miaka sita, mbele ya mama yake katika mji mtakatifu wa Madina nchini Saudi Arabia.
Habari ID: 3471835    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/02/09

TEHRAN (IQNA)- Ajuza mwenye umri wa miaka 75 nchini Saudi Arabia amefanikiwa kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu.
Habari ID: 3471820    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/01/27

TEHRAN (IQNA)-Mhubiri mashuhuri Saudi Arabia, Ahmed al-Amari, amefariki mjini Jeddah, Saudi Arabia.
Habari ID: 3471813    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/01/21

TEHRAN (IQNA)- Utawala wa kifalme wa Saudi Arabia umeanza mradi wa kuwatimua wakimbizi Waislamu wa jamii wa Rohingya ambao walikimbia mateso na mauaji ya kimbari katika nchi yao ya jadi, Myanmar.
Habari ID: 3471801    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/01/09

TEHRAN (IQNA) – Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Saudi Arabia zimesaini Mapatano ya Maelewano (MOU) kuhusu kushiriki Wairani katika ibada ya Hija mwaka huu wa 1440 Hijria na 2019 Miladia.
Habari ID: 3471777    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/12/19

TEHRAN (IQNA)- Uhusiano rasmi baina ya Utawala wa Kizayuni wa Israel na Utawala wa Kifalme Saudi Arabia unatazamiwa kutangazwa rasmi katika kipindi cha miezi michache ijayo.
Habari ID: 3471765    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/12/09

TEHRAN (IQNA)- Kamishna MKuu wa Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet ametoa wito wa kufanyika uchunguzi wa kimataifa kubaini mhusika wa mauaji ya mwandishi habari Msaudi Jamal Khashoggi.
Habari ID: 3471762    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/12/05

TEHRAN (IQNA)- Watoto zaidi ya 84,700 wa Yemen wamepoteza maisha kutokana na makali ya njaa na utapiamlo, tangu Saudi Arabia ianzishe vita dhidi ya nchi hiyo maskini jirani yake zaidi ya miaka mitatu iliyopita.
Habari ID: 3471748    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/11/22