IQNA

21:23 - September 15, 2019
News ID: 3472130
TEHRAN (IQNA) – Mkuu wa Shirika la Hija na Ziara za Kidini Iran Ali Reza Rashidian amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imefanya mazungumzo na Saudi Arabia kuhusu Wairani kuanza tena kutekeleza Ibada ya Umrah.

Akizungumza na waandishi habari mjini Tehran Jumapili, Rashidian amesema Iran imeifahamisha Saudi masharti ambayo yanapaswa kutumizwa kabla ya Wairani kuanza tena kutekeleza Ibada ya Umrah.

Amesema moja ya masharti hayo ni kuwa Saudi Arabia lazima itoe dhamana ya kuwaheshimu Wairani wanaotekeleza Ibada ya Umrah. Aidha amesema sharti jingine ni kuwa, Iran iruhusiwe kufungua ubalozi mdogo mjini Jeddah ili iweze kutoa huduma za kisheria na zisizo za kisiasa kwa raia wake wanaoshiriki katika Ibada ya Umrah. Aidha amesema sharti jingine ni kuwa Saudi Arabi iwaruhusu raia wake kutembelea Iran bila vizingiti.

Rashidian amesema kuwa, Saudi Arabia imetangaza kuwa tayari kuwapokea Wairani wanaoshirki katika Ibada ya Umrah. Ameongeza kuwa wakuu wa Saudia wana mpango wa kuwavutia Wairani milioni 30 watekeleze Ibada ya Umrah kila mwaka ifikapo mwaka 2030. 

Mkuu wa Shirika la Hija na Ziara za Kidini Iran amesema mwaka huu pekee Wairani milioni sita wako tayari kushiriki katika ibada ya Umrah. Rashidian amesema mwaka huu Wairani 88,555 walishiriki katika Ibadaha ya Hija kwa mafanikio.

Ikumbukwe kuwa, mnamo Septemba 2015, kulijiri msongamano mkubwa wakati wa ibada ya Hija katika eneo la Mina karibu na Makka ambapo duru zisizo rasmi zinasema Mahujaji 7,000 walipoteza maisha huku Saudia ikisisitiza ni watu 770 waliouawa katika msongamano huo. Iran ilitangaza kuwa mahujaji wake wapatao 465 walipoteza maisha katika maafa hayo ya Mina. Siku kadhaa kabla ya tukio hilo, Mahujaji 100 walipoteza maisha katika Msikiti Mtakatifu wa Makka, wakiwemo Wairani 11 baada ya winchi kuwaangukia wakati wanapotufu.

Maswali mwengi waliibuka kuhusu uwezo wa Saudi Arabia kusimamia zoezi la Hija ambapo mwaka jana Iran ilitaka usalama wa Mahujaji wake udhaminiwe. Kufuatia sisitizo hilo la Iran, Saudi Arabia mwaka uliofuata iliwazuia mahujaji Wairani kushiriki katika ibada ya Hija. Baada ya masharti ya Iran kudhaminiwa, Mahujaji Wairani walianza tena kutekeleza Ibada ya Hija mwaka 2017 lakini bado Iran na Saudia zilikuwa hazijafikia muafaka kuhusu Ibada ya Umrah.

3842254

Name:
Email:
* Comment: