Rais wa Iran
TEHRAN (IQNA)- Rais Ibrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekutana na kufanya mazungumzo hapa mjini Tehran na Faisal Mekdad, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Syria na kusema kuwa, nchi hiyo ya Kiarabu ipo mstari wa mbele katika mapambano na muqawama dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 3474648 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/12/07
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria jinai zilizofanywa na dikteta wa Iraq Saddam dhidi ya watu wa Iran na akasema: Saddam alikuwa akifanya jinai hizo kwa msukumo na uungaji mkono wa wanaojigamba kuwa watetezi wa haki za binadamu duniani.
Habari ID: 3474631 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/12/02
Spika wa Bunge la Iran
TEHRAN (IQNA)- Spika wa Majilisi ya Ushauri ya Kiislamu, Bunge la Iran, amesema haki za taifa la Iran zitarejeshwa tu iwapo kutafikiwa mapatano maziri na adilifu ambayo yatapalekea vikwazo kuondolewa.
Habari ID: 3474625 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/12/01
TEHRAN (IQNA)- Zahra Khalili, msichana mwenye ulemavu wa macho katika mji mkuu wa Iran, Tehran ni miongoni mwa wawakilishi wanne wa Iran katika mashindano yajayo ya Qur’ani ya kimataifa ya wanafunzi Waislamu.
Habari ID: 3474623 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/11/30
Rais wa Iran katika mazungumzo ya simu na Rais wa Ufaransa
TEHRAN (IQNA)- Rais Ibrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amemfahamisha Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa kuwa, Iran inataka kuona natija katika mazungumzo ya nyuklia yanayoendelea sasa Vienna Austria na kwamba lazima mazungumzo hayo yahitimishwe kwa Iran kuondolewa vikwazo.
Habari ID: 3474622 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/11/30
Rais wa Iran katika mkutano na Rais wa Uturuki
TEHRAN (IQNA)- Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema matatizo na changamoto za kieneo zinapaswa kutatuliwa na nchi za eneo na kwamba uingiliaji wa kigeni hausaidii lolote bali unachochea na kuvuruga zaidi hali ya mambo.
Habari ID: 3474617 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/11/29
TEHRAN (IQNA)- Mkuu wa Masuala ya Kimataifa wa Idara ya Mahakama ya Iran amesisitiza kuwa, mauaji ya kigaidi ya wanasayansi wa nyuklia ni jinai dhidi ya binadamu na ni ukiukaji wa sheria za kimataifa.
Habari ID: 3474614 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/11/28
TEHRAN (IQNA)- Hatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amezinasihi nchi za Ulaya kutotoa mhanga maslahi yao ya kitaifa kwa manufaa na malengo haramu ya watawala wa Marekani na utawala haramu wa Israel.
Habari ID: 3474601 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/11/26
Kiongozi Muadhamu kwa mnasaba wa kuanza Wiki ya Basiji
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametuma ujumbe wa maandishi kwa mnasaba wa Wiki ya Jeshi la Kujitolea la Basiji na kusema kuwa: Mabasiji mnapaswa kuwa watatuzi wa masuala yote ya nchi na ya taifa kwa kumtegemea na kutawakali kwa Mwenyezi Mungu, Mjuzi na Muweza wa kila siku.
Habari ID: 3474596 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/11/25
Rais wa Iran akimpokea Balozi wa Vatican
TEHRAN (IQNA)- Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa kutoa mazingatio kwa Mola Muumba na suala la umanaawi ni jambo la udharura mkubwa hii leo kwa jamii ya mwanadamu.
Habari ID: 3474593 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/11/23
TEHRAN (IQNA) - Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) ameipongeza Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kuitaja kama nguzo kuu na muhimu ya mrengo wa muqawama wa Wapalestina.
Habari ID: 3474587 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/11/21
TEHRAN (IQNA)- Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu y Iran ameelezea kusikitishwa kwake na kupoteza maisha na kujeruhiuwa idadi kubwa ya raia wa Burkina Faso .
Habari ID: 3474563 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/11/16
Rais Raisi wa Iran katika mkutano na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki
TEHRAN (IQNA)- Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekutana na kufanya mazungumzo hapa Tehran na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki na kusisitiza kuwa: Iran na Uturuki zinapasa kujiandaa kuimarisha uhusiano wa sasa kuelekea kwenye ushirikiano wa pande zote.
Habari ID: 3474561 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/11/15
TEHRAN (IQNA)- Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amepongeza hatua ya hivi karibuni ya Algeria kupinga utawala haramu wa Israel kupewa hadhi ya mwanachama mwangalizi katika Umoja wa Afrika.
Habari ID: 3474548 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/11/12
TEHRAN (IQNA)- Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limetoa taarifa na kusema kuwa, Aban 13 (Novemba 4) ambayo ni siku ya kupambana na ubeberu nchini Iran, bila ya shaka yoyote imebadilisha kabisa mlingano wa nguvu kieneo na kimataifa.
Habari ID: 3474517 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/11/05
TEHRAN (IQNA)- Hatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema kuwa Iran iko tayari kuingia kwenye mazungumzo ambayo matokeo yake ni kuondolewa vikwazo vyote na kwamba haikubali mazungumzo yasiyo na mwelekeo.
Habari ID: 3474516 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/11/05
TEHRAN (IQNA)- Operesheni maalumu na iliyotekelezwa wakati mwafaka na wanajeshi shupavu wa kikosi cha Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limefanikiwa kuzima jaribio la uharamia na wizi wa mafuta uliosimamiwa na manuwari ya kijeshi ya Marekani katika maji ya Bahari ya Oman.
Habari ID: 3474511 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/11/03
TEHRAN (IQNA)- Sheikh Mahmoud Shaltut wa Misri alikuwa miongoni mwa wanazuoni walioanzisha harakati ya kukurubisha madhehebu za Kiislamu na alitoa fatwa ya kihistoria kuhusu Ushia.
Habari ID: 3474491 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/10/30
TEHRAN (IQNA)- Matayarisho ya Mashindano ya 38 ya Kimataifa ya Qur'ani yameanza huku nchi kadhaa zikiwa tayaris zimeshatangaza kuwa tayari kushiriki.
Habari ID: 3474490 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/10/30
TEHRAN (IQNA)- Hatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema kuwa, harakati zinazofanywa na mabeberu kwa sasa zinalenga kuvuruga amani na usalama.
Habari ID: 3474488 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/10/29