IQNA

Rais Raisi alaani hujuma ya kigaidi Afghanistan, atuma rambirambi

16:57 - April 20, 2022
Habari ID: 3475146
TEHRAN (IQNA)- Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani hujuma ya kigaidi dhidi ya shule kadhaa katika mji mkuu wa Afghanistan, Kabul sambamba na kutuma salamu za rambirambi kwa familia za waliopoteza maisha.

Jana Jumanne kulijiri milipuko katika shule mbili zilizo katika mtaa wa Waislamu wa madheebu ya Shia mjini Kabul ambapo taarifa zinasema watu wasiopungua sita waliuawa na wengine 24 walijeruhiwa.

Akizungumza katika kikao cha baraza la mawaziri leo, Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema wanaobeba dhima ya mashambulio hayo ya kigaidi ni madola ambayo kwa jina la eti kudhamini usalama, yaliingilia mambo ya ndani ya Afghanistan na kusababisha ukosefu wa usalama.

Raisi pia ametoa wito kwa viongozi wa Afghanistan kutumia uwezo wao wote kuzuia hujuma za kigaidi ambazo zinawalenga watoto na wanafunzi wasio na hatia.

Rais wa Iran pia ameashiria fursa na changamoto zilizopo katika uhusiano wa kibiashara baina ya nchi za eneo na kusema Iran iko katika hali nzuri kibiashara lakini kuna haja ya kutumia fursa zilizopo kuimarisha uwezo wa sekta binafsi.

Serikali ya awamu ya 13 ya Iran tokea iingie madaraknai Agsoti 3, 2021 imekuwa ikitoa kipaumbele kwa suala la kuimarisha uhusiano wa kibiashara na nchi jirani, za Kiislamu na za Afrika.

135841

captcha