IQNA

Rais wa Iran: utawala wa Kizayuni wa Israel ni tishio kubwa kwa umma mzima wa Waislamu

12:28 - April 29, 2022
Habari ID: 3475183
TEHRAN (IQNA)- Rais Ebrahim Raeisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameupongeza mhimili wa muqawama au mapambano ya Kiislamu kwa kuuzuia utawala wa Kizayuni kutekeleza uharibifu zaidi katika eneo kama walivyofanya magaidi wakufurishaji.

Akizungumza Alhamisi jioni mjini Tehran wakati alipohutubu katika hadhara ya mabalozi wa nchi za Waislamu wanaoziwakilisha nchi zao hapa Iran alisema: "Kama si vijana waliojitolea wa harakati za muqawama katika umma wa Waislamu, Wazayuni wangekuwa wamezivuruga nchi za eneo kama walivyofanya magaidi wakufurishaji."

Ameongeza kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel ni tishio kubwa kwa umma mzima wa Waislamu.  Pamoja na hayo amesema kuunga mkono taifa linalodhulumiwa la Palestina ni nukta inayouunganisha umma huo.

Raisi ametoa kauli hiyo katika mkesha wa Ijumaa ya mwisho ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ambayo ilitangazwa na mwanzilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Imam Khomeini MA, kuwa ni Siku ya Kimataifa ya Quds.

Katika siku hii maelfu ya watu hujitokeza katika maandamano kote duniani kuunga mkono harakati za ukombozi wa ardhi ya Palestina iliyovamiwa na kukaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel.

Katika hotuba yake, Rais Raisi ametoa wito kwa Waislamu kote duniani kushiriki katika maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds.

Wakati huo huo Rais wa Iran ameonya kuhusu njama hatari za kujitanua za utawala haramu wa Israel ambao ni hatari kwa nchi za eneo na kwa utambulisho wa ulimwengu wa Kiislamu.  Kwa msingio huo amelaani aina yoyote ile ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel na kuongeza kuwa kujikurubisha na utawala huo bila shaka kutaibua hasira za Waislamu bilioni mbili kote duniani.  Amsema tawala ambazo zinaanizhsa uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wenye kiu ya damu kwa hakika zinalisha joka lililokaribu nao.

Ikumbukwe kuwa mwaka 2020 Umoja wa Falme za Kiarbau, Bahrain, Sudan na Morocco zilianzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel na hivyo kujiunga na Misri na Jordan ambazo ni nchi zingine za Kiarabu zilizo na uhusiano wa kawaida na utawala huo dhalimu unaozikoloni ardhi za Palestina.

136092

captcha