iran - Ukurasa 50

IQNA

TEHRAN (IQNA) - Mwanazuoni mtajika wa Kiislamu nchini Iran, Ayatullah Muhammad Yazdi, ameaga dunia leo na kurejea kwa Mola wake.
Habari ID: 3473438   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/12/09

Rais wa ya Iran katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria
TEHRAN (IQNA) - Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesemam kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itaendeleza maamuzi na irada ambayo imekuwa ikichukua katika kuiunga mkono serikali na taifa la Syria kama nchi muitifakii wake wa kistratejia na itakuwa bega kwa bega na Syria hadi kupatikana ushindi wa mwisho.
Habari ID: 3473435   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/12/08

TEHRAN (IQNA) - Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametuma ujumbe kwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa mnasaba wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kushikamana na Wananchi wa Palestina na kuitolea mwito jamii ya kimataifa kukabiliana na hatua za utawala wa Kizayuni wa Israel unaouwa watoto.
Habari ID: 3473415   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/12/02

TEHRAN (IQNA) - Wabunge wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) wamelitaka Shirika la Atomiki la Iran kuzalisha urani iliyorutubishwa kwa zaidi ya asilimia 20 kwa ajili ya matumizi ya amani.
Habari ID: 3473412   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/12/01

TEHRAN (IQNA)- Nchi na viongozi mbalimbali duninani wameendelea kulaani mauaji ya mwanasayansi wa nyuklia wa Iran na kusisitiza kuchukuliwa hatua waliohusika na jinai hiyo.
Habari ID: 3473405   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/11/29

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametilia mkazo wajibu wa kutiwa adabu na kupewa adhabu isiyoepukika wote waliofanya na kuamrisha mauaji ya kigaidi ya mwanasayansi wa Kiirani, Dk. Mohsen Fakhrizadeh.
Habari ID: 3473403   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/11/28

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran
TEHRAN (IQNA) - Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif amelaani vikali hujuma hiyo ya kigaidi na kuongeza kuwa, kuna dalili nzito zinazoonyesha kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel ulihusika katika mauaji ya Mohsen Fakhrizadeh ambaye alikuwa Mkuu wa Shirika la Utafiti na Ubunifu katika Wizara ya Ulinzi ya Iran.
Habari ID: 3473401   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/11/28

Siku kama ya leo miaka 1241 iliyopita inayosadifiana na tarehe 10 Rabiuthani mwaka 201 Hijria, alifariki dunia Bibi Fatima Maasuma A.S, binti wa Imam Musa bin Jaafar A.S mmoja wa wajukuu watukufu wa Bwana Mtume Muhammad SAW.
Habari ID: 3473397   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/11/26

Mkuu wa zamani wa Chuo Kikuu cha Kiislamu Ghana
TEHRAN (IQNA) – Jerry Rawlings, Rais wa zamani wa Ghana ambaye amefariki hivi karibuni akiwa na umri wa miaka 73, alikuwa mwanasiasa Mkristo ambaye aliathiriwa na kuiga baadhi ya fikra za Mapinduzi ya Kiislamu.
Habari ID: 3473388   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/11/24

Zarif katika Twitter baada ya
TEHRAN (IQNA) - Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Tehran kwa mara nyingine tena inatangaza kwamba iko tayari kushirikiana na nchi za eneo hili kwa ajili kulinda na kufanikisha manufaa ya pamoja.
Habari ID: 3473344   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/11/09

TEHRAN (IQNA) – Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amenukulu aya za Qur’ani Tukufu katika Surah An-Naziat katika kufafanua kushindwa Donald Trump katika uchaguzi wa rais Marekani mwaka huu.
Habari ID: 3473342   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/11/08

Rais Rouhani wa Iran
TEHRAN (IQNA) - Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema taifa hili halijalishwi wala kushughulishwa na ni nani atakayeibuka mshindi katika uchaguzi wa rais wa Marekani uliofanyika jana Jumanne.
Habari ID: 3473328   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/11/04

TEHRAN (IQNA)- Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewatumia ujumbe marais wa nchi za Kiislamu akiwapongeza kwa mnasaba wa kuadhimisha Maulidi na siku ya kuzaliwa Mtume wa mwisho wa Mwenyezi Mungu na Nabii wa rehma, upendo na amani, Muhammad SAW.
Habari ID: 3473324   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/11/03

TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei atahutubu kwa njia ya televisheni kwa mnasaba wa maadhimisho ya kukumbuka siku ya kuzaliwa (Maulid) Mtume Muhammad SAW na pia uzawa wa mjukuu wake, Imam Jaafar Swadiq AS.
Habari ID: 3473318   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/11/01

TEHRAN (IQNA) - Mshauri wa sera za kigeni wa Spika wa Bunge la Iran ameashiria mauaji ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ambaye aliuawa kigaidi kufuatia amri ya rais Donald Trump wa Marekani na kusema, Trump ni gaidi nambari moja duniani.
Habari ID: 3473315   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/31

TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu ametilia mkazo udharura wa kuundwa kituo maalumu cha za Kiislamu kwa ajili ya kukabiliana na maafa katika ulimwengu wa Kiislamu.
Habari ID: 3473312   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/31

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu akiwahutubu vijana Wafaransa
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameeleza kushangazwa kwake na undumakuwili wa Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa kwa kulikingia kifua jarida la Charlie Hebdo la nchini hiyo ya Ulaya kwa kuchapisha tena vibonzo vya kumvunjia heshima Mtume Muhammad SAW, kwa kisingizio cha uhuru wa kujieleza.
Habari ID: 3473306   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/29

TEHRAN (IQNA) - Mkutano wa 34 wa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu unatazamiwa kuanza Alhamisi kwa njia ya intaneti ambapo mada kuu itakuwa 'Ushirikiano wa Kiislamu Wakati wa Maafa na Majanga'.
Habari ID: 3473300   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/27

TEHRAN (IQNA- Balozi Mdogo wa Ufaransa mjini Tehran, Florent Aydalot, ameitwa katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kukabidhiwa malalamiko ya Iran kuhusu sisitizo la serikali ya Ufanrasa la kuwaunga mkono waliochapisha katuni zilizomvunjia heshima Mtume Muhammad SAW.
Habari ID: 3473299   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/27

Spika wa Bunge la Iran
TEHRAN (IQNA) - Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu, Bunge la Iran, amesema nuru ya Mtume Mtukufu wa Uislamu, SAW, haiwezi kuzimwa kwa njama za maadui wa Kiislamu na kwamba njama hizo zitarejea kuwadhuru wao wenyewe.
Habari ID: 3473296   Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/26