Rais Hassan Rouhani
TEHRAN (IQNA) - Rais Hassan Rouhani wa Iran Jamhuri ya Kiislamu amesema nchi hii katu haitasitisha uuzaji wa mafuta ghafi yake ya petroli katika soko la kimataifa pamoja na kuwepo mashinikizo na vikwazo vipya vya Marekani.
Habari ID: 3471936 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/04/30
TEHRAN (IQNA) – Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kundi lenye misimamo mikali la Timu B linamchochea Rais Donald Trump wa Marekani aanzishe vita dhidi ya Iran.
Habari ID: 3471932 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/04/29
Spika wa Bunge la Iran
TEHRAN (IQNA) -Spika wa Bunge la Iran, Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu, ulimwengu wa Kiislamu leo unakabiliwa na tatizo la misimamo mikali na utakfiri.
Habari ID: 3471931 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/04/28
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, uhusiano wa mataifa mawili ya Iran na Pakistan ni wa moyoni uliokita mizizi vyema na kusisitiza kuwa, uhusiano huo unapaswa kuimarishwa kadiri inavyowezekana hata kama maadui wa mataifa haya mawili watachukizwa na hilo
Habari ID: 3471924 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/04/23
TEHRAN (IQNA)- Mashindano ya Tatu ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran maalumu kwa ajili ya wanawake yamemalizika Ijumaa mjini Tehran.
Habari ID: 3471914 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/04/13
TEHRAN (IQNA)- Harakazi za mapambano ya Kiislamu Iraq ambazo zimekuwa mstari wa mbele katika vita dhidi ya ugaidi zimelaani vikali, hatua ya uhasama ya mtawala wa Marekani Donald Trump ya kuliweka Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) nchini Iran katika orodha ya makundi ya kigaidi.
Habari ID: 3471910 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/04/11
TEHRAN (IQNA)- Fainali za Mashindano ya 36 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zimeanza rasmi Jumatano alasiri katika halfa iliyofanyika mjini Tehran.
Habari ID: 3471909 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/04/10
TEHRAN (IQNA) – Nchi 27 zitawakilishwa katika Mashindano ya 6 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran maalumu kwa ajili ya wanafunzi wa shule.
Habari ID: 3471905 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/04/08
TEHRAN (IQNA) – Washiriki wa Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wameanza kuwasili nchini.
Habari ID: 3471904 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/04/08
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA)-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, Marekani inapinga mchakato wa demokrasia nchini Iraq.
Habari ID: 3471903 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/04/07
Kiongozi wa Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwepo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika harakati ya Tauhidi (Kumpwekesha Mwenyezi Mungu) ni chanzo kikuu cha uhasama wa Marekani na vibaraka wake kama vile ukoo wa Aal Saud.
Habari ID: 3471897 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/04/03
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, katika ujumbe kwa munasaba wa kuanza mwaka mpya wa 1398 Hijiria Shamsia, ametuma salamu za pongezi za Nowuruz (Nairuzi) na pia salamu kwa munasaba Wilada ya Imam Ali AS kwa wananchi wa Iran na hasa familia za mashahidi na majeruhi wa vita na amelitakia taifa la Iran mwaka wenye furaha, saada, afya ya kimwili na mafanikio ya kimaada na kimaanawi na ameutaja mwaka mpya kuwa mwaka wa "kustawi uzalishaji".
Habari ID: 3471884 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/03/21
Rais Rouhani katika ujumbe wa Nowruz
TEHRAN (IQNA) - Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mapema Alhamisi ametuma ujumbe kwa kunasaba wa kuanza mwaka mpya wa 1398 Hijria Shamsiya na kusema mwaka 1397 ulikuwa mwaka wa mafanikio makubwa ya taifa la Iran katika nyuga mbali mbali na kuongeza kuwa, kwa yakini taifa la Iran litapata ushindi na litavuka matatizo yaliyopo.
Habari ID: 3471883 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/03/21
TEHRAN (IQNA)-Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelaani vikali hujuma za kigaidi zilizolenga misikiti miwili jana mjini Christchurch New Zealand na kupelekea Waislamu wasiopungua 49 kuuawa shahidi wakiwa katika Sala ya Ijumaa.
Habari ID: 3471878 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/03/16
TEHRAN (IQNA) – Waziri wa Elimu wa Iran Sayyid Mohammad Bathayi amesema takribani wanafunzi zaidi ya milioni mbili nchini Iran wanashiriki darsa za kuhifadhi Qur'ani.
Habari ID: 3471871 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/03/11
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuhusu kuwepo uthabiti na amani nchini Myanmar. Aidha amesisitiza kuwa wakimbizi Waislamu wa jamii ya Rohingya warejeshwe haraka na kwa usalama katika makazi yao nchini Myanmar.
Habari ID: 3471869 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/03/09
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Khamenei amesisitiza umuhimu wa utunzaji misitu na kusema umuhimu wa kupanda miti ni jambo ambalo linapaswa kuhimizwa ili liwe utamaduni wa umma.
Habari ID: 3471866 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/03/07
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA) Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema wakati alipoonana na kuzungumza na Rais Bashar al Assad wa Syria hapa mjini Tehran Jumatatu kwamba, Iran inalihesabu suala la kuiunga mkono Syria kuwa ni sawa na kuunga mkono muqawama (mapambano ya Kiislamu) na inaona fakhari kwa jambo hilo.
Habari ID: 3471853 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/02/26
TEHRAN (IQNA)- Jumuiya ya Kimataifa ya Maulama wa Kiislamu imelaani vikali mkutano wa hivi karibuni baina ya maafisa wa ngazi za juu wa nchi za Kiarabu na Waziri Mkuu wa Utawala wa Kizayuni wa Israel huko Warsaw, Poland.
Habari ID: 3471846 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/02/19
TEHRAN (IQNA) Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Jumatano ametoa ujumbe muhimu sana kwa taifa la Iran kwa jina la "Hatua ya Pili ya Mapinduzi" kwa mnasaba wa maadhimisho ya miaka 40 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Habari ID: 3471841 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/02/14