Kwa mujibu wa mwandishi wa Shirika la Kimataifa la Habari za Qur'ani IQNA, karibu Waislamu 800 wamekimbilia ndani ya Kanisa Katoliki kwenye mji wa Carnot wa kusini-maghairbi mwa nchi huyo. Magaidi wa Kikristo sasa wamewataka Waislamu hao waondoke la sivyo kanisa hilo litateketezwa kwa moto na wao wakiwa ndani. Magaidi wa Kikristo wanaendelea kuwaua Waislamu Jamhuri ya Afrika ya Kati huku idadi kubwa ya Waislamu wakilazimika kukimbilia katika nchi jirani kwa khofu ya kuuliwa na magaidi hao. Hivi karibuni shirika la kutetea haki za binaadamu Human Rights Watch limetaka hatua za haraka zichukuliwe kwa lengo la kuzuia mauaji ya halaiki ya Waislamu huko Jamhuri ya Afrika ya Kati. Waislamu ni takribani asilimia 15 ya watu milioni 4.6 katika Jamhuri ya Afrika ya Kati. Ripoti zinasema kuwa magenge ya Wakristo wenye misimamo mikali wamewaua maelfu ya Waislamu nchini humo huku mamia ya maelfu wakilazimika kukimbilia katika nchi jirani. Kuna askari 1,600 wa Ufaransa na maelfu ya askari wengine wa kulinda amani kutoka nchi za Kiafrika huko Jamhuri ya Afrika ya Kati lakini wameshindwa kuzuia mauaji ya Waislamu yanayofanywa na magenge ya Wakristo.