Sayyid Nasrullah amesema, kuendelea kuwepo kundi la kitakfiri la Daesh (ISIL) katika eneo hili ni kwa maslahi ya Uturuki na Marekani. Akizungumza siku Jumatatu, ameongeza kuwa vita vya Marekani naya waitifaki wake dhidi ya Daesh vina lengo la kuwawekea matakfiri wa Daesh mstari mwekundu ili ‘wasikaribie Saudi Arabia, Jordan na Erbil (mji mkuu wa eneo lenye mamlaka ya ndani la Kurdistan nchini Iraq).
Sayyid Nasrullah amesema, anaamini kuwa Uturuki haikujiunga katika vita vya Marekani na waitifaki wake dhidi ya Daesh pasina kuhakikishiwa kulindwa maslahi yake. Amesema sharti ambalo Uturuki imeliweka ili kushiriki katika vita vinavyoongozwa na Marekani dhidi ya Daesh ni hakikisho kuwa Marekani itaipindua serikali ya Syria.
Kiongozi wa Hizbullah amesema hivi sasa harakati ya Muqawama ya Lebanon iko tayari kuilinda nchi hiyo na kukabiliana na njama za matakfiri.
Hivi karibuni Sayyid Nasrallah alijitokeza akiwa amevalia sare za kijeshi katika eneo la Bonde la Bekaa kusini mwa Lebanon ambapo alikagua oparesheni za Hizbullah katika eneo hilo.../mh