IQNA

Iran yalaani hatua ya Daesh (ISIL) kumuwa rubani wa Jordan

22:25 - February 04, 2015
Habari ID: 2811515
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelaani vikali hatua ya mgaidi wa kundi la Daesh (ISIL) kumuwa kinyama rubani wa Jordan aliyekuwa ametekwa nyara na kundi hilo.

Katika taarifa, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Bi. Marzieh Afkham amelaani vikali kitendo hicho kilicho dhidi ya ubinaadmau cha kundi la kitakfiri la Daesh. Halikhadhalika ametoa salamu zake za rambi rambi kwa familia, serikali na watu wa Jordan kufuatia msiba huo. Aidha ametoa wito wa kuchukuliwa hatua kali dhidi ya ugaidi na na pia ametaka kusikuwepo undumakuwili katika kukabiliana na makundi ya kigiaid.
Ikumbukwe kuwa hiyo jana Jumanne, magaidi wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu la Iraq na Sham yaani Daesh (ISIL) lilionyesha mkanda wa video wakati wa kuchomwa kwa moto Moaz al-Kassasbeh rubani wa Jordan, aliyetekwa nyara miezi miwili iliyopita na kundi hilo. Ukatili huo umezusha hasira kote duniani. Baada ya kuoneshwa mkanda huo wa mauaji ya kutisha, Jordan kwa upande wake imelipiza kisasi kwa kuwanyonga wanachama wawili wa kundi la kitakfiri la al Qaeda waliokuwa wakizuiliwa katika jela za nchi hiyo.../mh

2808354

captcha