IQNA

Wanafunzi Waislamu New York wakabiliwa na chuki

14:18 - March 09, 2015
Habari ID: 2954393
Wanafunzi Waislamu katika jiji la New York wamekuwa wakikabiliwa na miamala ya kibaguzi na kuvunjiwa heshima kutokana na kuongezeka hisia za chuki dhidi ya dini Tukufu ya Uislamu nchini Marekani.

Wanafunzi wa Kiislamu katika shule za New York wamekuwa wakilalamikia kushtadi vitendo vya utumiaji mabavu dhidi yao. Aidha katika shule nyingine za serikali katika eneo la Astoria kwenye Kaunti ya Queens New York pia wanafunzi Waislamu hususan wanafunzi wa kike wamekuwa wakilalamikia na vitendo vya bughudha na maudhi kama hivyo wanavyofanyiwa kila leo. Ahmad Jamil Mkuu wa Taasisi ya Waislamu wa Marekani amesema kuwa, vitendo vya kibaguzi dhidi ya Waislamu vinaendelea nchini humo. Hii ni katika hali ambayo ripoti nyingi zimechapishwa kuhusu vitendo na miamala hiyo mibovu ya kibaguzi wanayofanyiwa Waislamu katika miji mbalimbali ya Marekani likiwemo jiji la New York. Itakumbukwa kuwa wanachuo watatu Waislamu katika jimbo la Carolina kaskazini na Muislamu mwingine katika jimbo la Texas hivi karibuni waliuliwa kikatili kwa kupigwa risasi.../mh

2945736

captcha