IQNA

Rais Hassan Rouhani

Hujuma ya Saudia nchini Yemen ni kosa la kistratejia

6:15 - May 10, 2015
Habari ID: 3277848
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, hujuma ya kinyama ya Saudi Arabia katika jirani ya Yemen ni kosa la kistratejia.

Rais Rouhani amesema hayo Jumamosi mjini Tehran kwa mnasaba wa “Wiki ya Hilali Nyekundu” na kubainisha kuwa, utawala ambao haufahamu vyema masuala ya kisiasa ulimwenguni, na siku zote umekuwa ukitatua mambo ya nchi yake kwa kutumia dola za Kimarekani umeishambulia Yemen kwa dhana kwamba, kwa kutumia mabomu utaweza kuifanya nchi yake iwe na nguvu na hivyo kufikia malengo yake katika Mashariki ya Kati. Rais wa Iran amehoji kwamba, kama mashambulio hayo yangefanywa kwa nchi nyingine isiyokuwa Yemen, Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu lingefanya nini? Rais Rouhani ameongeza kuwa, Yemen ambayo ni nchi ya ulimwengu wa tatu na ambayo inakabiliwa na matatizo chungu nzima, imeshambuliwa kinyama na jirani yake Saudia na kupelekea maelfu ya watu wasio na hatia kuuawa na kujeruhiwa huku nyumba zao zikibomolewa. Rais Rouhani amesema bayana kwamba, taifa la Iran lipo pamoja na wananchi madhulumu na wasio na ulinzi wa Yemen na kwamba, Shirika la Hilali Nyekundu la Iran limepaza sauti ya kuwasaidia wananchi hao na kwamba Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu nalo linapaswa kuwasaidia

wananchi hao wanaotaabika.../mh

3274603

captcha