Sayyid Nasrallah amesema utawala wa Israel haupaswi kudhani kuwa Hizbullah inajishughulisha na oparesheni dhidi ya makundi ya magaidi nchini Syria. Ameonya kuwa utawala wa Israel utapata jibu kali ukijaribu kuvamia Lebanon kijeshi.
Kiongozi wa Hizbullah amesema pamoja na kuwepo propaganda zote dhidi ya harakati hiyo ya muqawama, imeweza kuppata mafanikio makubwa katika eneo la Qalamoun katika mpaka wa Lebanon na Syria.
Amesema wanamapambano wa Hizbullah wamekomboa maeneo mengi mpakani ambayo yalikuwa yakishikilia na kundi la kitakfiri la al-Nusra. Kuhusu kundi la kitakfiri la Daesh (ISIL, ISIS), kiongozi wa Hizbullah amesema kundi hilo lilianzia Iraq, kisha kuelekea Syria. Nasrallah amesema Daesh ilijitenga na kundi la kigaidi la al-Qaeda, kundi ambalo liliundwa na mashirika ya kijasusi ya Marekani, Saudia na Pakistan. Kuhusu hujuma ya kijeshi ya Saudia nchini Yemen, amesema utawala wa Saudia haujafanikiwa katika malengo. Ammesema Saudia imeua raia na kuharibu maeneno mengi ya nchi hiyo jinai ambazo hata magenge ya wahalifu hawawezi kutenda.../mh